“INAONEKANAJE KUWASAIDIA WENGINE KUWA ZAIDI KAMA KRISTO?”
Katika mwongozo huu mfupi, mchungaji Mark Dever anajibu maswali ya nani, nini, wapi, lini, kwa nini, na jinsi ya kukuza wanafunzi wa Kristo—kuwasaidia wengine kumfuata Yesu. Kwa kufuata mfano wa Maandiko, kitabu hiki kinafafanua jinsi mahusiano ya kukuza wanafunzi yanavyopaswa kufanyika katika muktadha wa kanisa la mahali. Kinatufundisha jinsi ya kukuza utamaduni wa kufanya wanafunzi kama sehemu ya kawaida ya maisha yetu ya kila siku.
"Ukitaka kuhamia ngazi nyingine katika maisha yako ya kiroho na uongozi, chukua muda kusoma kitabu hiki. Kitabu hiki sio tu cha kibiblia , bali cha kivitendo na kinacho someka. Msisitizo wake juu ya kanisa la mahali na nafasi yake katika kuwafanya wengine kuwa wanafunzi ndio unao kitofautisha na vitabu vingine. Kisome na uwashirikishe wengine."Ronnie Floyd, Rais, Mkutano wa Wabaptisti wa Kusini; Mchungaji Kiongozi,
Kanisa la Msalaba, Springdale, Arkansas
“Iwapo unamfahamu Mark Dever, basi unajua kwamba amejitolea sana katika kukuza wanafunzi wa Kristo. Kitabu hiki kinaangazia kile kinachomsukuma na jinsi anavyowafundisha wengine. Jiandae kwa kubadilika kwa maisha unapokisoma kitabu hiki!”
CONRAD MBEWE, Mchungaji, Kabwata Baptist Church, Lusaka, Zambia
“Kila mfuasi wa Kristo anapaswa kukisoma kitabu hiki! Ni kitabu bora zaidi nilichowahi kusoma kuhusu kukuza wanafunzi wa Kristo.”
JANI ORTLUND, Makamu wa Rais Mtendaji, Renewal Ministries; mwandishi wa vitabu Fearlessly Feminine na His Loving Law, Our Lasting Legacy.
MARK DEVER (PhD, Chuo Kikuu cha Cambridge) ni mchungaji mkuu wa Kanisa la Capitol Hill Baptist huko Washington, DC, na rais wa 9Marks. Ameandika zaidi ya vitabu kumi na viwili, vikiwemo Nine Marks of a Healthy Church kilichouzwa sana, na hutoa hotuba kwenye mikutano duniani kote.
Kufanya Wanafunzi: Jinsi ya Kuwasaidia Wengine Kumfuata Yesu
Mark Dever
We do not provide refunds or accept returns for purchased books. However, we are committed to addressing any issues related to manufacturing defects in the books you receive.