JE, MASHEMASI WANAWEZAJE KUHAMASISHA HUDUMA KANISANI?
Mashemasi ni muhimu kwa ustawi wa kanisa—lakini mara nyingi kuna
mkanganyiko kuhusu maelezo ya kazi yao kulingana na Maandiko. Ni ipi nafasi
waliyopewa na Mungu katika ushirika wa kanisa la mahali, na wanahusikaje na
ujumbe wa jumla wa kanisa?
Katika kitabu hiki kifupi, Matt Smethurst anaeleza kuwa mashemasi ni watumishi
wa mfano walioitwa kushughulikia mahitaji ya dhahiri, kuandaa na kuhamasisha
huduma mbalimbali, kuhifadhi umoja wa kanisa, na kusaidia huduma za wazee wa
kanisa. Kwa kusahihisha dhana potofu zilizozoeleka, Smethurst anatoa mwongozo
wa vitendo wa jinsi ya kuwateua na kuwawezesha mashemasi kufanya kazi yao, ili
kusaidia makanisa kustawi.
“Kama ningekuwa na nafasi ya kurudi nyuma na kuchagua kitabu kimoja cha
kujitayarisha kwa changamoto nyingi za huduma ambazo kanisa letu limekabiliana nazo mwaka huu, ningechagua hiki.”
— BOBBY SCOTT, Mchungaji Mwenza, Community of Faith Bible Church, South Gate, California.
“Shauku yangu kuu katika vitabu kuhusu utawala wa kanisa ni kwamba waandishi
wajenge hoja zao kwa msingi wa maelezo ya kina ya Biblia, badala ya kufuata mapokeo ya kidhehebu au maoni binafsi. Smethurst amefanikisha hili kwa ufasaha. Kwa mpangilio wazi na maarifa ya kuvutia, anarejesha kusudi la Biblia kwa mashemasi.”
— ALEXANDER STRAUCH, mwandishi wa “Biblical Eldership” na “Paul’s Vision for the
Deacons”
“Kanisa limehitaji kwa muda mrefu kitabu hiki ambacho ni cha kibiblia wazi, rahisi
kusoma, na chenye mafundisho ya kiutendaji. Mashemasi kinapaswa kubaki kuwa
maandishi ya msingi kwa muda mrefu, katika kanisa la mahali na katika taasisi za elimu ya juu.”
— MALCOM B. YARNELL III, Profesa Mtafiti wa Theolojia, Southwestern Baptist
Theological Seminary; Mchungaji Mwalimu, Lakeside Baptist Church, Granbury, Texas.
MATT SMETHURST ni mhariri mkuu wa The Gospel Coalition. Amewahi kuhudumu
kama shemasi na mzee wa kanisa katika Third Avenue Baptist Church huko Louisville,
Kentucky, na kwa sasa yuko katika mchakato wa kuanzisha kanisa jipya huko
Richmond, Virginia.
Mashemasi: Namna Gani Wanatumikia Nakulitia Nguvu Kanisa
MATT SMETHURST
We do not provide refunds or accept returns for purchased books. However, we are committed to addressing any issues related to manufacturing defects in the books you receive.