JE, KANISA LINAJILINDI VIPI DHIDI YA INJILI ZA UONGO?
Kila wiki, makanisa mengi duniani husoma Biblia lakini hukosa kufikia ujumbe
wake mkuu—na hivyo huishia kufundisha injili za uongo mara kwa mara.
Mojawapo ya ngao muhimu zaidi dhidi ya hatari hii ni ufahamu wa theolojia ya
kibiblia: kusoma Biblia kwa mtazamo wa ujumbe wake wa msingi, ambao
unakamilika ndani ya Yesu Kristo.
Kwa kuanzia na mfumo wa kuelewa mfululizo wa hadithi ya Biblia na kisha
kueleza kanuni za msingi za kuipa kipaumbele kufundisha ujumbe huu, kitabu
hiki kinalenga kusaidia makanisa kulinda ukweli wa Injili.
“Ikiwa unatafuta rasilimali inayofafanua na kutumia theolojia ya kibiblia kwa usahihi,
basi hiki ndicho kitabu chako. Nimeshangazwa na jinsi mafundisho imara
yalivyowekwa katika kitabu kifupi kama hiki.”
MIGUEL NÚÑEZ, Mchungaji Mkuu, International Baptist Church of Santo Domingo
“Rasilimali yenye msaada mkubwa kwa wachungaji, walimu, na waumini wa kawaida.”
THOMAS R. SCHREINER, Profesa wa Tafsiri ya Agano Jipya na Theolojia ya
Kibiblia, The Southern Baptist Theological Seminary
“Katika kitabu hiki kilichojaa mifano yenye nguvu na inayofumbua macho, Roark na
Cline wanatoa hoja za kushawishi kwamba kuelewa jinsi mfululizo wa hadithi ya Biblia
unavyomhusu Yesu Kristo kunamwezesha kila mwamini kumtumikia kwa mujibu wa
makusudi ya Mungu. Soma kitabu hiki na ujionee mwenyewe!”
CONRAD MBEWE, Mchungaji, Kabwata Baptist Church; Kansela, The African
Christian University, Lusaka, Zambia
NICK ROARK (MDiv, Chuo cha Theolojia cha Southeastern Baptist) ni mchungaji wa
Franconia Baptist Church huko Alexandria, Virginia. Hapo awali, aliwahi kuhudumu
kama sehemu ya timu ya wachungaji wa Capitol Hill Baptist Church huko Washington, DC.
ROBERT CLINE ni mkurugenzi mkuu wa mafunzo na mtaala katika Bodi ya Kimataifa
ya Ujumbe ya Jumuiya ya Wabaptisti wa Kusini.
Theolojia Ya Kibiblia: Jinsi Kanisa Linavyo Fundisha Injili kwa Uaminifu
NICK ROARK & ROBERT CLINE
We do not provide refunds or accept returns for purchased books. However, we are committed to addressing any issues related to manufacturing defects in the books you receive.