KWANINI UNAPASWA KUJIUNGA NA KANISA?
Kuwa mshirika wa kanisa ni sehemu muhimu, lakini mara nyingi hupuuzwa,
ya maisha ya Kikristo. Hata hivyo, kwa nyakati za sasa, kuna mwelekeo wa
kuepuka dini zilizoandaliwa na kuonyesha chuki au hofu ya kujitolea, hasa
kwa taasisi.
Jonathan Leeman anashughulikia masuala haya kwa maelezo ya moja kwa
moja kuhusu ushirika wa kanisa na kwa nini ni muhimu. Akilipa kanisa la
mahali heshima linayostahili, Leeman ameweka msingi wa hoja yenye nguvu
kwa ajili ya kujitoa kwa mwili wa Kristo wa mahali.
“Kimejaa mawazo ya kiutendaji na hoja nzuri zitakazotusaidia kuwaponya Wakristo
katika tamaduni yetu ya leo dhidi ya mzio wa ushirika wa kanisa, mamlaka ya
kichungaji, uwajibikaji wa maisha, na mipaka yoyote kwa uhuru wao wa kibinafsi.”
TIM KELLER, Mchungaji Mkuu, Redeemer Presbyterian Church, New York City
“Kifupi, cha kipekee, cha kuvutia, na, zaidi ya yote, cha kibiblia. Haya ni maelezo nautetezi wa ushirika wa kanisa ambayo umekuwa ukitafuta.”
MARK DEVER, Mchungaji Mkuu, Capitol Hill Baptist Church, Washington, DC
“Leeman anatukumbusha kuwa ushirika wa kanisa si chaguo bali ni hitaji. Kitabu hiki
kina mtindo wa moja kwa moja na chenye kuchochea fikra, lakini wakati huohuo
kimejaa injili ya neema.”
THOMAS SCHREINER, Profesa wa Tafsiri ya Agano Jipya, The Southern Baptist
Theological Seminary
JONATHAN LEEMAN (MDiv, Southern Baptist Theological Seminary) ni mshirika
wa Capitol Hill Baptist Church huko Washington, DC, na mwandishi wa The Church and the Surprising Offense of God’s Love. Pia anahudumu kama mkurugenzi wa uhariri wa 9Marks Ministries na mhariri wa jarida lake la mtandaoni, eJournal.
Ushirika wa Kanisa: Jinsi Ulimwengu Unavyojua Nani Anamwakilisha Yesu
JONATHAN LEEMAN
We do not provide refunds or accept returns for purchased books. However, we are committed to addressing any issues related to manufacturing defects in the books you receive.