Kitu chochote kinachoonekana ni nuru. Kwa hiyo husema, Amka, wewe usinziaye, ufufuke katika wafu, naye Kristo atakuangaza. (Waefeso 5:14)
Yesu alipomwamuru Lazaro afufuke kutoka kwa wafu, alitiije amri hiyo? Andiko la Yohana 11:43 linasema, “[Yesu] akapaaza sauti kwa nguvu, Lazaro, njoo huku nje.” Hiyo ilikuwa amri kwa mtu aliyekufa. Mstari unaofuata unasema, “Akatoka yule aliyekuwa amekufa, amefungwa sanda mikono na miguu” (Yohana 11:44).
Lazaro aliwezaje kufanya hivyo? Mtu aliyekufa anatiije amri ya kuishi tena? Jibu linaonekana kuwa: Amri hubeba uwezo wa kutengeneza maisha mapya. Kutii amri kunamaanisha kufanya kile ambacho watu walio hai wanafanya.
Njia ya kutii amri ya kuzaliwa ni kupata zawadi ya uhai na pumzi, kisha kumlilia Mungu kwa imani, shukrani, na upendo.
Hii ni muhimu sana. Amri ya Mungu, “Ufufuke kutoka kwa wafu!” hubeba ndani yake nguvu tunayohitaji ili kuitii. Hatuitii kwa kuumba uhai huo. Tunaitii kwa kufanya kile ambacho watu walio hai hufanya — Lazaro alitoka. Aliifufuka. Alitoka kwenda kwa Yesu. Wito wa Mungu huleta uhai. Tunaitikia kwa uwezo wa kile wito huleta.
Katika Waefeso 5:14, Paulo anasema, “Amka, wewe usinziaye, ufufuke katika wafu, naye Kristo atakuangaza.” Je, unatiije amri ya kuamka kutoka usingizini? Ikiwa nyumba yako ina sumu ya monoksidi ya kaboni ndani yake, na mtu analia, "Amka! Jiokoe! Toka nje!” hautii kwa kujiamsha. Sauti kubwa, amri kubwa, yenye nguvu yenyewe ndio huamsha. Unatii kwa kufanya yale ambayo watu walio macho hufanya wakati wa hatari. Unaamka na kutoka kwenye nyumba. Wito huleta kuamka. Unaitikia kwa nguvu ya kile wito ulichounda — kuamka.
Ninaamini kuwa haya ndiyo maelezo ya kwa nini Biblia inasema mambo ya kutatanisha kuhusu kuzaliwa upya; yaani, ni lazima tujipatie mioyo mipya, lakini kwamba ni Mungu ambaye huumba moyo mpya. Kwa mfano:
Kumbukumbu la Torati 10:16: “Tahirini mioyo yenu!” Kumbukumbu la Torati 30:6 “BWANA atautahiri moyo wako.”
Ezekieli 18:31: “Jifanyieni moyo mpya na roho mpya!” Ezekieli 36:26 "Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu."
Yohana 3:7: “Lazima uzaliwe mara ya pili.” 1 Petro 1:3 : “Mungu alitufanya tuzaliwe mara ya pili.”
Amri ya Mungu, “Ufufuke kutoka kwa wafu!” hubeba ndani yake nguvu tunayohitaji ili kuitii. Hatuitii kwa kuumba uhai huo.
Njia ya kutii amri ya kuzaliwa ni kupata kwanza zawadi ya kimungu ya uhai na pumzi, na kisha kufanya kile ambacho watu wanaoishi na kupumua hufanya: kumlilia Mungu kwa imani na shukrani na upendo. Amri ya Mungu inapokuja na uumbaji, nguvu za kubadilisha za Roho Mtakatifu, huleta uzima. Na tunaamini na kufurahi na kutii.
Comments