“Msijisumbue, mkisema, Tutakula nini? au 'Tutakunywa nini?' au 'Tuvae nini?' Kwa maana hayo yote hutafuta sana watu wa mataifa; na Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.” (Mathayo 6:31-32)
Yesu anataka wafuasi wake wawe huru na hali ya kuwa na wasiwasi. Katika Mathayo 6:25–34, anatoa hoja zisizopungua saba zilizokusudiwa kuondoa wasiwasi wetu. Anaorodhesha vyakula na vinywaji na mavazi, na kisha kusema, “Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote” (Mathayo 6:32).
Ni lazima Yesu anamaanisha kwamba kujua kwa Mungu kunaambatana na kutamani kwake kutimiza uhitaji wetu. Anasisitiza kuwa tuna Baba. Na Baba huyu ni bora kuliko baba yeyote wa duniani.
Nina watoto watano. Ninapenda kukidhi mahitaji yao. Lakini kujua kwangu ni kudogo kuliko kujua kwa Mungu katika angalau namna tatu.
Kwanza, sasa hivi sijui mtoto wangu yeyote yuko wapi. Ningeweza kukisia. Wako majumbani mwao au kazini au shuleni, wakiwa na afya njema na salama. Lakini wanaweza kuwa wamelala kando ya barabara wakiwa na mshtuko wa moyo.
Yesu anamaanisha kwamba kujua kwa Mungu kunahusiana na kutamani kwake kutimiza uhitaji wetu, akisisitiza kuwa tuna Baba ambaye ni bora kuliko baba yoyote duniani.
Pili, sijui wana nini moyoni mwao wakati wowote. Naweza kukisia mara kwa mara. Lakini wanaweza kuwa wanahisi woga fulani au kuumizwa au hasira au tamaa au uchoyo au furaha au matumaini. Siwezi kuiona mioyo yao. Hata wao hawaijui mioyo yao kikamilifu.
Tatu, sijui mustakabali wao wa yajayo. Hivi sasa wanaweza kuonekana vizuri na thabiti. Lakini kesho huzuni kubwa inaweza kuwapata.
Hii inamaanisha kuwa siwezi kuwa kwao sababu kubwa ya wao kutokuwa na wasiwasi. Kuna mambo ambayo yanaweza kuwa yanawatokea sasa, au yanaweza kutokea kesho, ambayo hata siyajui. Lakini ni tofauti kabisa na Baba yao wa mbinguni. Baba yetu wa mbinguni! Anajua kila kitu kuhusu sisi, tulipo, sasa na kesho, ndani na nje. Anaona kila hitaji.
Zaidi ya hilo, ana shauku kubwa ya kutimiza mahitaji yetu. Kumbuka “zaidi” ya Mathayo 6:30, “Ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, yaliyo hai leo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi zaidi?”
Lakini Baba yetu wa mbinguni anajua kila kitu kuhusu sisi, na mahitaji yetu yote.
Ongeza pia uwezo wake kamili wa kufanya kile anachotamani kufanya (analisha mabilioni ya ndege kila saa, duniani kote, Mathayo 6:26).
Kwa hiyo ungana nami katika kuamini ahadi ya Yesu ya kukidhi mahitaji yetu. Hivyo ndivyo Yesu anatoa wito anaposema, “Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnayahitaji hayo yote.”
Comments