top of page

Faraja Yetu Inapotoka

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read

[Pilato] Akaingia tena ndani ya makao yake makuu na kumwambia Yesu, “Unatoka wapi?” Lakini Yesu hakumpa jibu. Kwa hiyo Pilato akamwambia, "Je, utakaa kimya, hutazungumza nami? Je, hujui kwamba nina mamlaka ya kukuachilia na mamlaka ya kukusulubisha?" Yesu akamjibu, “usingelikuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama haingekuwa umepewa kutoka juu.” (Yohana 19:9–11)

 

Mamlaka ya Pilato ya kumsulubisha Yesu hayakumtisha Yesu. Kwanini?

 

Si kwa sababu Pilato alikuwa anadanganya. Sio kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kumsulubisha Yesu. Alikuwa nayo. 

 

Badala yake, mamlaka haya hayakumtisha Yesu kwa sababu yalikuwa ya kutegemea, alikuwa amepewa. Yesu alisema, “wewe ulipewa mamlaka kutoka juu.” Hii inamaanisha kuwa Pilato ana mamlaka ya kweli. Si pungufu. Lakini zaidi.

 

Kwa hiyo, ni kwa namna gani hii isiwe ya kutisha? Si tu kwamba Pilato ana mamlaka ya kumuua Yesu. Lakini ana mamlaka ya kumuua aliyopewa na Mungu.

 

Hii haimtishi Yesu kwa sababu mamlaka ya Pilato juu ya Yesu yako chini ya mamlaka ya Mungu juu ya Pilato. Yesu anapata faraja yake wakati huu si kwa sababu mapenzi ya Pilato hayana nguvu, bali kwa sababu mapenzi ya Pilato yanaongozwa. Si kwa sababu Yesu hayuko mikononi mwa hofu ya Pilato, bali kwa sababu Pilato yuko mikononi mwa Baba yake Yesu.

 

Hii inamaanisha kwamba faraja yetu haitokani na udhaifu wa maadui zetu, bali kutokana na utawala wa enzi wa Baba yetu juu ya nguvu zao. 

 

Hii ndiyo hoja ya Warumi 8:35-37. Dhiki na shida na mateso na njaa na utupu na hatari na upanga haviwezi kututenganisha na Kristo kwa sababu “katika mambo haya yote sisi ni zaidi ya washindi kupitia yeye aliyetupenda.” 

 

Pilato ana mamlaka, Herode ana mamlaka, Wanajeshi wana mamlaka, Shetani ana mamlaka, Lakini hakuna aliye na mamlaka huru, ya kujitegemea, Usiogope. Wewe ni wa thamani kwa Baba yako mwenye enzi kuu.

Pilato (na maadui wote wa Yesu — na wetu) walikusudia mabaya. Lakini Mungu alikusudia mema (Mwanzo 50:20). Maadui wote wa Yesu walikusanyika pamoja na mamlaka waliyopewa na Mungu ili "kufanya chochote ambacho mkono wa Mungu na mpango wa Mungu ulikuwa umepanga kutokea tangu awali" (Matendo 4:28). Walitenda dhambi. Lakini kupitia dhambi zao Mungu aliokoa.

 

Kwa hiyo, msiogopeshwe na maadui zenu ambao wanaweza kuua mwili tu (Mathayo10:28). Siyo tu kwa sababu hiki ndicho wanachoweza kufanya (Luka 12:4), bali pia kwa sababu kinafanyika chini ya mkono wa uangalizi wa Baba yako.

 

Je, shomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hakuna hata mmoja wao anayesahaulika mbele za Mungu. Kwanini, hata nywele za kichwa chako zimehesabiwa zote. Usiogope; wewe una thamani zaidi kuliko shomoro wengi. (Luka 12:6–7)

 

Pilato ana mamlaka. Herode ana mamlaka. Wanajeshi wana mamlaka. Shetani ana mamlaka. Lakini hakuna aliye na mamlaka huru, ya kujitegemea. Mamlaka yao yote yanatokana na chanzo kingine. Yote yanatii mapenzi ya Mungu. Usiogope. Wewe ni wa thamani kwa Baba yako mwenye enzi kuu. Wa thamani zaidi kuliko ndege wasiosahaulika.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page