top of page

Huduma na Hofu ya Mwanadamu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read

“Usiogope kwa sababu yao, kwa maana mimi niko pamoja nawe kukuokoa, asema Bwana." (Yeremia 1:8)

 

Kikwazo kikubwa katika kumtumikia Bwana, hasa miongoni mwa vijana, ni hofu ya kukataliwa na kupingwa. 

 

Mawazo ya aina zote huingia akilini kuhusu jinsi baadhi ya watu watachukia jinsi tunavyotenda au kuzungumza. Watu wanaweza kutokubaliana au kukasirishwa nasi. Naweza kufanya makosa na kukosolewa.

 

Hofu ya mwanadamu ni kikwazo kikubwa katika huduma.

 

Kwa hiyo, Mungu anasema, Usihofu, kwa sababu nitakuwa pamoja nawe na nitakuokoa. Uwepo na kibali cha Mungu ni vya thamani zaidi kuliko sifa zote za wanadamu. Na Mungu anasema kwamba, ukiwa ndani ya magumu na kupitia matatizo yako yote, Mimi nitakuokoa. Utashinda mwishoni. Utakuwa zaidi ya mshindi. 

 

Uwepo na kibali cha Mungu ni vya thamani zaidi kuliko sifa za wanadamu— Yeye ndiye anayekuhifadhi na kukuokoa, na atakuwa pamoja nawe daima.

Na jambo hilo hilo limeahidiwa kwetu sote katika Kristo Yesu leo:

 

  • "[Mungu] amesema, ‘Sitamwacha kamwe wala kumtelekeza.’ Kwa hivyo tunaweza kusema kwa ujasiri, ‘Bwana ni msaidizi wangu; sitaogopa; mwanadamu anaweza kunifanyia nini?’" (Waebrania 13:5-6)

  • "Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani anayeweza kuwa dhidi yetu?" (Warumi 8:31)

 

Kwa hivyo Mungu alimwambia kijana Yeremia, na Mungu anawaambia vijana leo ambao anawaita kumtumikia — na sisi sote — “Usiseme, ‘Mimi ni kijana tu’” — au mimi ni mzee sana, au mimi si chochote (Yeremia 1:7). Kwanini?

 

  • Kwasababu maisha yako yamejikita katika makusudi yasiyoyumbishwa na ya enzi ya Mungu. Umechaguliwa na kutakaswa na kuumbwa na kuteuliwa kwa kusudi kuu.

  • Kwasababu mamlaka ya Mungu, si yako mwenyewe, ndiyo yanayosimamia utumishi wako na kuongea kwako.

  • Na kwa sababu Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nawe kukuokoa katika majaribu yako yote.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page