top of page

Imani Ndogo Kuliko Zote

Haitegemei mapenzi ya mwanadamu au bidii, lakini inategemea Mungu, ambaye ana rehema. (Warumi 9:16)

 

Hebu tuweke wazi mwanzoni mwa mwaka kwamba yote tutakayopata kutoka kwa Mungu mwaka huu, kama waumini katika Yesu, ni rehema. Raha au maumivu yoyote yatakayotupata yote yatakuwa rehema. Hii ndiyo sababu Kristo alikuja ulimwenguni: “ili Mataifa wapate kumtukuza Mungu kwa ajili ya rehema zake” (Warumi 15:9). Tulizaliwa mara ya pili “kulingana na rehema zake nyingi” (1 Petro 1:3). Tunaomba kila siku "ili tupate rehema " (Waebrania 4:16); na sasa “tunangojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo iletayo uzima wa milele” (Yuda 1:21). Ikiwa Mkristo yeyote atathibitika kuwa mwaminifu, ni “kwa rehema za Bwana [yeye] ni mwaminifu” (1 Wakorintho 7:25). 

 

Yote tutakayopata kutoka kwa Mungu mwaka huu, kama waumini katika Yesu, ni rehema, iwe raha au maumivu. 

Katika Luka 17:5–6, mitume wanamsihi Bwana, “Utuongezee imani!” Naye Yesu anasema, “Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeweza kuuambia mkuyu huu, 'Ng’oka, ukapandwe baharini', nao ungewatii." Kwa maneno mengine, suala katika maisha na huduma zetu za Kikristo sio nguvu au wingi wa imani yetu, kwa sababu sio hiyo inayong'oa miti. Mungu ndiye afanyae hivi.  Kwa hiyo, imani ndogo kabisa inayotuunganisha na Kristo itashirikisha nguvu zake zote kwa mahitaji yako yote.


Lakini vipi kuhusu nyakati ambazo unafanikiwa kumtii Bwana? Je, utiifu wako unakutoa kwenye kundi la muombaji wa rehema? Yesu anatoa jibu katika mistari inayofuata ya Luka 17:7–10.

 

“Je, kuna yeyote kati yenu aliye na mhudumu anayelima au anayechunga kondoo atamwambia anapoingia kutoka shambani, ‘Njoo mara moja na uketi mezani’? Je, hatamwambia, 'Niandalie chakula cha jioni, vaa vizuri, na unihudumie wakati nikila na kunywa, kisha nawe ule na kunywa'? Je, anamshukuru mhudumu kwa sababu ametenda aliyoamriwa? Vivyo hivyo nanyi, mtakapokuwa mmefanya yote mliyoagizwa, semeni, 'Sisi tu wauhudumu wasiofaa kitu; tumefanya tu yaliyokuwa wajibu wetu.’”

 

Imani ndogo inayotuunganisha na Kristo itatufanya tushiriki nguvu zake zote kwa mahitaji yetu yote.

Kwa hiyo, nahitimisha hivi, utii kamili na imani ndogo zaidi hupata kitu kimoja kutoka kwa Mungu: rehema. Mbegu ndogo ya haradali ya imani inapata rehema ya nguvu za Mungu za kuhamisha miti. Na utiifu usio na dosari hutuacha tutegemee tu rehema.


Hoja ni hii: Haijalishi wakati au aina ya rehema ya Mungu, kamwe hatupandi juu ya hadhi ya wapokeaji wa rehema. Daima tunategemea kabisa kile ambacho hatustahili. 


Kwa hiyo tujinyenyekeze wenyewe na kushangilia na “tumtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake!”

Opmerkingen


bottom of page