top of page

Ipande Milima ya Mafumbo ya Mungu



Makala imeandikwa na John Piper

Mwanzilishi na Mwalimu, desiringGod.org


Nimesoma waandishi na kusikia wasemaji wanaojaribu kugeuza ujinga wetu juu ya njia za Mungu kuwa msingi mkuu wa mshangao wetu na ibada. Kwa kawaida hufanya hivyo kwa kutumia neno chanya fumbo kurejelea vilindi na urefu wa Mungu ili kwamba tunapaswa kuguswa na kushangazwa na kustaajabishwa kwa jinsi tusivyomjua Mungu.


Muda wote niliiona hali hii kuwa ya kupotosha.  Sivutiwi na watu wanaofanya hivi. Mtazamo wa Paulo, kwa mfano, ni tofauti sana. Angesema kwamba Mungu hutukuzwa zaidi tunapopigwa na butwaa na kumstaajabia na kumwabudu na kujinyenyekeza kwa furaha kwa sababu ya yale tunayoyajua kumhusu, si kwa sababu ya yale ambayo hatujui kumhusu.


Paulo anasema Mungu hutukuzwa tunapomwabudu kwa furaha kwa sababu ya yale tunayoyajua kumhusu, si kwa sababu ya yale ambayo hatujui.

Kustaajabishwa na kushangazwa kwako katika safu ya milima kunaweza kutegemea mtazamo wako kutoka chini ya vilima, ambapo unaweza kuona safu hiyo ikipanda na kutoweka kwenye mawingu ya chini. Au huenda ikatokana na safari za miaka mingi kwenye safu ya milima ili kugundua kwamba kila unapofika juu yaa kilele kimoja kirefu sana, safu nyingine nzima ya milima hupaa mbele yako na juu yako.


Sio heshima kubwa kwa Mungu kuyatumia maisha yako katika vilima, kuandika insha na mashairi juu ya kiasi gani hujui kinachotokea juu ya mstari wa wingu. Afadhali zaidi kumruhusu Mungu aweke mkono wako katika mkono wa Paulo - au yeyote kati ya waandishi wake wengine waliovuviwa - na kisha uyatumie maisha yako yote kupanda pamoja naye kwenye njia za juu za ufunuo.


“Haitafutiki na Haichunguziki”?

Mojawapo ya vifungu vilivyoeleweka vibaya na vilivyotumiwa vibaya sana katika maandishi ya Paulo ni sehemu kuu ya kilele mwishoni mwa Warumi 1–11:


Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki na njia zake zisivyotafutikana!

“Ni nani aliyefahamu mawazo ya Bwana, 

Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake? 

“Au ni nani aliyempa chochote ili arudishiwe?”


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake, na kwa ajili yake. Atukuzwe milele. Amina. (Warumi 11:33-36)


Jambo kuu ni hili hapa: Paulo haandiki kustaajabishwa huku kunakoongezeka wa utajiri wa Mungu badala ya kuuonyesha utajiri huo, lakini kwa sababu ametoka tu kuuweka wazi utajiri huo katika sura kumi na moja za ufunuo wa kushangaza. Anapaa juu kwa sababu ya kile alichotoka kukifunua , si kwa sababu ya yote yaliyosalia kufunikwa. Maneno haya ya mshangao yanakuja mwishoni mwa sura kumi na moja ambamo Paulo ametupeleka katika kina na kimo cha njia za Mungu kupita vile ambavyo yeyote kati yetu alifikiria inawezekana.


Kusoma tu vifungu vitatu viliyotangulia kunaichanganya akili kuhusu njia za Mungu. Sio kwa sababu ziko nyuma ya wingu la kutokujua, lakini kwa sababu zimefunuliwa kama zisizotarajiwa kabisa na zisizoeleweka na za kushtua na za kumtukuza Mungu. Paulo anaelezea mipango ya Mungu kwa Wayahudi na Mataifa:


Kama vile ninyi [Wa Mataifa] wakati fulani mlivyokuwa waasi kwa Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa sababu ya kutotii kwao [Wayahudi], hivyo nao Waisraeli wamekuwa waasi ili kwamba wao nao sasa waweze wameasi kupata rehema kwa ajili ya rehema za Mungu kwenu. Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye uasi, ili apate kuwarehemu wote. (Warumi 11:30-32)


Chukua dakika tano kutafakari vifungu hivyo, na utatoka mara ya kwanza umepigwa na butwaa, na kisha kustaajabu, si kwa sababu umeachwa gizani, bali kwa sababu nuru inang’aa sana huwezi kuamini kile unachokiona.


“Haitafutiki” Lakini Imeletwa kwenye Nuru

Paulo anaeleza ufunuo wake wa njia za Mungu kuwa hazitafutiki mara nyingine tena. Na uhakika sio kwamba anatuacha chini ya vilima bila ujuzi.


Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii: ili niwahubirie watu wa Mataifa kuhusu   utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo , na kuweka wazi kwa kila mtu siri hii  iliyokuwa imefichwa tangu zamani katika Mungu, aliyeumba vitu vyote. (Waefeso 3:8-9)


Andiko hili halimaanishi, “Pole, enyi watu, utajiri wa Kristo uko katika giza la siri, na hauwezi kufunuliwa. Andiko linasema kinyume chake: “Mungu aliniita,” Paulo asema, “akanipa kipaji cha kuidhihirisha siri hiyo! Mambo ninayoandika juu ya Kristo ni utajiri wa Kristo usiotafutika!”


Hayawezi kutafutika katika maana tatu:

  1. Yamefichwa ndani ya Mungu kwa muda mrefu—lakini si hivyo tena!

  2. Yanaweza kujulikana tu kwa ufunuo wa kiungu, si hekima ya kibinadamu - na Paulo anauandika ufunuo huo.

  3. Daima kutakuwa na mengi ya kuona unapopanda katika maana ya ufunuo uliovuviwa, na kisha kuingia katika Milima ya Himalaya ya mbinguni.


Kujua Kinachopita Maarifa

Jambo hili la mwisho linathibitishwa katika sala ya Paulo katika sura inayofuata ya Waefeso. Anaomba kwamba sisi tuwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Kristo; na kujua upendo huu unaopita fahamu , ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu. ( Waefeso 3:18-19 )


Hivi ndiyo ilivyo! Kwa sababu ya ufunuo wa ajabu wa Mungu wa njia zake katika Kristo—kupitia maandishi ya mtume Paulo—tumepewa “kujua upendo wa Kristo unaopita maarifa.” Tunapelekwa juu zaidi na zaidi katika safu za milima ya maajabu ya Mungu ili kwamba kwa kweli tujue yale ambayo yalikuwa hayajulikani, na kuona kwamba milima inazidi kuongezeka zaidi.


Mungu anaheshimishwa tunapokubali mwaliko wake wa kutuongoza katika hukumu na njia zake zisizotafutika wala kuchunguzika.

Wa-Sherpa wenye Miguu ya Uhakika

Paulo hakuwa mmoja wa wale watu ambao wanatosheka kuishi chini ya vilima vya ufunuo, huku akizidisha ufasaha juu ya thamani ya "siri" iliyo juu ya mawingu ya chini. Paulo alijua kwamba Mungu alimpa wito wa kutojificha , bali kuhubiri “utajiri wa Kristo usiotafutika.”


Paulo alijua kwamba Mungu haheshimiwi tunapokaa bondeni, tukiisifu sana thamani ya fumbo ambalo halijagunduliwa. Mungu anaheshimiwa tunapokubali mwaliko wake wa kutuongoza katika hukumu zake zisizotafutika na njia zake zisizochunguzika - tunapowatendea waandishi wa Maandiko kama Wa-Sherpa wenye miguu ya uhakika katika milima ya Himalaya ya ufunuo wa Mungu.

Comments


bottom of page