top of page

Jinsi ya Kufurahia Neno la Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read

Maneno yako ni matamu kwa ladha yangu, matamu kuliko asali kinywani mwangu! (Zaburi 119:103)

 

Usipunguze Ukristo kuwa suala la madai, maazimio, na nguvu ya kutaka. Ni suala la kile tunachopenda, kile tunachofurahia, kile chenye ladha nzuri kwetu. 

 

Yesu alipoingia ulimwenguni, wanadamu waligawanyika kulingana na kile walichopenda. "Nuru imekuja ulimwenguni, na watu walipenda giza kuliko nuru" (Yohana 3:19). Wenye haki na waovu wanatofautishwa na kile wanachokifurahia — ufunuo wa Mungu katika Yesu, au njia ya dunia. 

 

Kwa hivyo mtu anaweza kuuliza: Ninawezaje kufurahia neno la Mungu? Jibu langu lina sehemu mbili: 

 

  1. Omba kwa ajili ya ladha mpya kwenye ulimi wa moyo wako; 

  2. Tafakari juu ya ahadi za kushangaza za Mungu kwa watu wake.

 

Hakuna mtu anayetaka kuwa makapi yasiyo na mizizi; sote tunatamani kupata nguvu kutoka kwenye mto wa ukweli na kuwa watu wenye matunda na manufaa.

Mwandishi huyohuyo wa zaburi aliyesema, “Maneno yako ni matamu kwa ulimi wangu” (Zaburi 119:103), alisema awali, “Fungua macho yangu, nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako” (Zaburi 119:18). Aliomba hivi, kwasababu kuwa na macho ya kiroho kuona utukufu, au kuwa na ladha takatifu kwenye ulimi wa moyo, ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hakuna mtu anayetamani kwa asili, na kumfurahia, Mungu na hekima yake.


Lakini unapokuwa umeomba, na hata unapokuwa unaomba, tafakari juu ya faida ambazo Mungu anaahidi kwa watu wake na juu ya furaha ya kuwa na Mungu Mwenyezi kama msaidizi wako sasa na milele. Zaburi 1:3-4 inasema kwamba mtu anayefikiria juu ya neno la Mungu “ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, unaozaa matunda yake kwa wakati wake, na majani yake hayanyauki. Katika yote afanyayo, anafanikiwa. Waovu si hivyo, bali ni kama makapi yanayopeperushwa na upepo."

 

Usipunguze Ukristo kuwa madai na maazimio— ni suala la kile tunachopenda, kile tunachofurahia, na kile chenye ladha nzuri kwa roho zetu.

Nani asiyefurahia kusoma kitabu ambacho kusoma kwake kungeweza kumgeuza mtu kutoka kuwa makapi yasiyofaa na kuwa mwerezi mkubwa wa Lebanoni, kutoka jangwa la vumbi la Texas hadi bustani ya matunda ya Hawaii? Hakuna mtu ambaye kwa undani anataka kuwa makapi — yasiyo na mizizi, yasiyo na uzito, yasiyo na maana. Sote tunataka kupata nguvu kutoka kwenye mto wenye kina wa ukweli na kuwa watu wenye matunda na wenye manufaa.

 

Mto huo wa ukweli ni neno la Mungu, na watakatifu wote wakuu wamefanywa wakuu kwa huo.

1 Kommentar


Gast
26. März

Asante kwa kazi zenu nzuri kwa kuleta somo la leo. Hii ni baraka

Gefällt mir
100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page