Mkitumikia kwa nia njema, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa jema lolote afanyalo mtu, atapokea hilo kutoka kwa Bwana, kwamba ni mtumwa au ni mtu huru. (Waefeso 6:7-8)
Fikiria mambo haya matano kutoka kwa Waefeso 6:7–8 kuhusiana na kazi yako.
1) Wito wa kuishi kwa kumzigatia Bwana.
Hii inashangaza ikilinganishwa na jinsi tunavyoishi kwa kawaida. Paulo anasema kwamba kazi zetu zote zinapaswa kufanywa kama kazi kwa ajili ya Kristo, sio kwa ajili ya msimamizi yeyote wa kibinadamu. Toeni utumishi kwa nia njema “ kama kwa Bwana na si kwa wanadamu.”
Hii ina maana kwamba tutamfikiria Bwana katika kile tunachofanya kazini. Tutauliza, Kwanini Bwana angependa hili lifanyike? Je, Bwana angetaka hili lifanyike? Bwana angetaka hili lifanyike lini? Je, Bwana atanisaidia kulifanya hili? Je, hii itakuwa na matokeo gani kwa heshima ya Bwana? Kwa maneno mengine, kuwa Mkristo maana yake ni kuishi na kufanya kazi kwa kumzigatia Bwana.
2) Wito wa kuwa mtu mwema.
Kuishi kwa kumzigatia Bwana kunamaanisha kuwa mtu mwema na kufanya mambo mema. Paulo asema, “Kwa nia njema [toa huduma] . . . chochote kizuri anachofanya mtu yeyote.” Yesu alisema kwamba tunapoacha nuru yetu iangaze, watu wataona “matendo yetu mema ” na kumtukuza Baba yetu aliye mbinguni (Mathayo 5:16).
Paulo anasema kazi zetu zote zinapaswa kufanywa kama kazi kwa ajili ya Kristo, sio kwa msimamizi wa kibinadamu.
3) Nguvu ya kufanya kazi nzuri kwa waajiri wa kidunia wasiojali.
Kusudi la Paulo ni kuwawezesha Wakristo, kwa nia iliyozingatia Bwana, kuendelea kufanya mema kwa wasimamizi wasiojali. Je, unaendeleaje kufanya vizuri katika kazi wakati bosi wako anakupuuza au hata kukukosoa? Jibu la Paulo ni: acha kumfikiria bosi wako kama msimamizi wako mkuu, na anza kufanya kazi kwa ajili ya Bwana. Fanya hivi katika majukumu uliyopewa na msimamizi wako wa kidunia.
4) Kukutia moyo kwamba hakuna jambo jema linalofanywa bure.
Labda sentensi ya kustaajabisha kuliko yote ni hii: “Lolote jema ambalo mtu atendalo, atalipokea kutoka kwa Bwana.” Hii inashangaza. Kila kitu! "Chochote kizuri ambacho mtu yeyote anafanya." Kila jambo dogo unalolifanya ambalo ni jema linaonekana na kuthaminiwa na kulipwa na Bwana.
Naye atakulipa kwa hilo. Sio kwa maana kwamba umestahili chochote — kana kwamba unaweza kumweka kwenye deni lako. Anakumiliki, na kila kitu katika ulimwengu. Hatumdai chochote. Lakini kwa hiari, anachagua kutupa thawabu kwa mambo yote mema tunayofanya kwa imani.
Kila jambo jema unalofanya linaonekana na kuthaminiwa na Bwana, ambaye atakulipa kwa hiari yake kwa mambo mema tunayofanya kwa imani.
5) Kutia moyo kwamba hadhi duni duniani sio kizuizi cha thawabu kubwa mbinguni.
Bwana atakulipa kwa kila jema unalofanya — "iwe ni mtumwa au ni mtu huru." Msimamizi wako anaweza kufikiri wewe si mtu wa maana — mtumwa tu, kwa mfano. Au hata pengine hajui upo. Hiyo haijalishi. Bwana anajua upo. Na mwishoni hakuna huduma ya uaminifu itakayokuwa ya bure.
Comments