top of page

Jinsi ya Kutubu

Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:9)

 

Hisia mbaya zisizoeleweka kwamba wewe ni mtu mbaya si sawa na kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi. Kuhisi kuoza sio sawa na toba.


Asubuhi ya leo nilianza kuomba, na nikajiona sistahili kuzungumza na Muumba wa ulimwengu. Ilikuwa hisia isiyo ya wazi ya kuhisi kutostahili. Basi nikamwambia hivyo. Sasa je?


Hakuna kilichobadilika hadi nilipoanza kuwa wazi kweli na kwa kina juu ya dhambi zangu. Hisia mbaya zinaweza kuwa na manufaa ikiwa zinakuongoza kwenye hatia ya dhambi mahususi. Lakini hisia zisizo wazi za kuwa mtu mbaya mara nyingi huwa hazisaidii sana.


Ukungu wa kutostahili unahitaji kuchukua sura kuwa nguzo za wazi za kutotii. Kisha unaweza kuyaelekezea kidole, kutubu, kuomba msamaha, na kulenga kwa bazooka yako ya injili ili kuyapasua kabisa.


Hisia mbaya zisizoeleweka kwamba wewe ni mtu mbaya si sawa na kuhukumiwa kwa dhambi. Kuhisi kuoza sio toba.

Kwa hiyo nilianza kukumbuka amri ninazovunja mara kwa mara. Hizi ndizo zilizokuja akilini:

  • Mpende Mungu kwa moyo, roho, akili na nguvu zako zote. Sio 95%, lakini 100%. (Mathayo 22:37)

  • Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Uwe na hamu ya kutaka mambo yaende vizuri kwake kama vile unavyotamani mambo yaende vizuri kwako. (Mathayo 22:39)

  • Fanya mambo yote bila kunung'unika. Hakuna kunung'unika — ndani au nje. (Wafilipi 2:14)

  • Mtwike yeye fadhaa zako zote, ili usilemewe nazo tena. (1 Petro 5:7)

  • Sema tu mambo ambayo yanayowapa wengine neema — hasa wale walio karibu nawe zaidi. (Waefeso 4:29)

  • Ukomboeni wakati. Usipoteze dakika, au kulega kulega. (Waefeso 5:16)


Huu ni mwisho wa madai yangu yoyote ya utakatifu! Nimevunjika.


Hili ni baya zaidi kuliko hisia zisizoeleweka na za hovyo. Ah, lakini sasa adui anaonekana. Dhambi ni mahususi. Zimetoka mafichoni. Ninazitazama machoni. Sinung'uniki kuhusu kuhisi vibaya. Ninaomba msamaha kwa Kristo kwa kutofanya mambo mahususi ambayo aliamuru.


Nimevunjika, na nina hasira juu ya dhambi yangu. Nataka kuiua dhambi, sio mimi. Sina mawazo ya kujiua. Mimi ni mchukia-dhambi na muuaji-dhambi. (“Yafisheni yaliyo ya kidunia ndani yenu,” Wakolosai 3:5; “Yafisheni matendo ya mwili,” Warumi 8:13.) Nataka kuishi. Ndiyo maana mimi ni muuaji — wa dhambi yangu!

 

Katika pambano hili, nasikia ahadi, “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Amani inaongezeka. 

 

Sasa, maombi yanaonekana kuwa yanawezekana, sahihi, na yenye nguvu tena.


Nimevunjika na nina hasira juu ya dhambi yangu. Nataka kuiua dhambi, sio mimi. Mimi ni mchukia na muuaji wa dhambi.

Comments


bottom of page