top of page

Jivike silaha kupitia Ahadi hizi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read

"Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

 

Paulo anaposema kuua matendo ya mwili “kwa Roho” (Warumi 8:13), ninachukulia kwamba anamaanisha tunapaswa kutumia silaha pekee katika silaha za Roho inayotumika kuua; yaani, upanga, “ambao ni neno la Mungu” (Waefeso 6:17)

 

Kwa hiyo, mwili unapokuwa karibu kuongozwa katika tendo la dhambi kwa hofu au tamaa fulani, tunapaswa kuchukua upanga wa Roho na kuua hofu hiyo na tamaa hiyo. Kwa uzoefu wangu, hiyo inamaanisha kukata mzizi wa ahadi ya dhambi kwa nguvu ya ahadi kuu. 

 

Kwa mfano, ninapoanza kutamani raha za ngono zisizofaa, neno ambalo mara nyingi limekata mzizi wa tamaa hii ni, “Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu” (Mathayo 5:8). Nakumbuka raha nilizopata kwa kumwona Mungu waziwazi kutoka katika dhamiri isiyo na doa; na nakumbuka ladha mbaya ya dhambi, na kwa kupitia hilo, Mungu ameua nguvu ya dhambi.

 

Kuwa na ahadi zinazofaa wakati wa majaribu ni ufunguo mmoja wa vita vya mafanikio dhidi ya dhambi. 

 

Lakini kuna nyakati ambapo hatuna neno linalofaa kabisa kutoka kwa Mungu katika akili zetu. Na hakuna muda wa kutafuta ahadi maalum kwenye Biblia. Kwa hivyo, sote tunahitaji kuwa na hazina ndogo ya ahadi za jumla tayari kwa kutumia wakati wowote hofu au tamaa zinapotishia kutupotosha.

 

Kuwa na ahadi zinazofaa wakati wa majaribu ni ufunguo wa kushinda ahadi za dhambi kwa nguvu ya ahadi kuu za Mungu.

Hapa kuna ahadi nne ambazo mara nyingi natumia katika kupambana na dhambi:

 

Isaya 41:10, Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. 

 

Wafilipi 4:19, "Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu."

 

Na ahadi iliyopo katika Wafilipi 3:8, "Nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya faida isiyo na kiasi ya kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu."

 

Na, bila shaka, Mathayo 5:8, Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu.

 

Endelea kuongeza katika hazina ya silaha zako za ahadi mara kwa mara. Lakini usiache kuzitazama zile ambazo Mungu amekubariki nazo katika maisha yako. Fanya haya yote. Kuwa tayari kila wakati iwapo utatakiwa kuzitumia zile za zamani. Na kila asubuhi tafuta ahadi mpya za kutembea nazo kwa ajili ya siku nzima.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page