top of page

Krismasi Ni Siri Kubwa Kuliko Zote

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 4, 2024
  • 4 min read


Makala imeandikwa na David Mathis

Mhariri Mtendaji, desiringGod.org


Ni saa iliyogawanya historia katikati.


Hadi Krismasi ile ya kwanza, alikuwa, tangu milele, Mwana wa Mungu na nafsi ya pili ya Uungu. Alikuwa wakala wa furaha wa Mungu katika uumbaji (Yohana 1:3 ; Wakolosai 1:16; Waebrania 1:2), na tangu mwanzo wa wakati, alikuwa akiutegemeza ulimwengu kila wakati (Wakolosai 1:17; Waebrania 1:3) .


Lakini basi yakaja mabadiliko makubwa - nyongeza iliyobarikiwa - katika kiini cha uhalisia. Neno alifanyika mwili (Yohana 1:14). Mungu akawa mwanadamu. Muumba mwenyewe alikuja kama kiumbe, Mwandishi aliingia katika Hadithi yake kama mhusika. Bila kuacha namna yoyote ya kuwa Mungu, aliyachukua yote yanayomaanisha kuwa mwanadamu.


"Bila kuacha namna yoyote ya kuwa Mungu, aliyachukua yote yanayomaanisha kuwa mwanadamu." #umwilisho #kufanyika-mwili

Ukweli huu wa kuvutia, katikati ya kile tunachosherehekea wakati wa Krismasi, tunachoita "umwilisho," yaani "kufanyika mwili" kwa Mwana wa Mungu - Mungu mwenyewe akichukua mwili na damu na ubinadamu wetu wote. Krismasi ni wakati anapoongeza ubinadamu kwenye uungu wake, na kufanya hivyo ili aweze kutuokoa kutoka kwenye uasi wetu unaoangamiza roho, na kutujaza na furaha ya milele ambayo tulifanywa.


Muungano wa Kifumbo

Ni ufunuo mtukufu, na pia ni fumbo kuu. Hili ndilo fumbo kuu zaidi katika historia yote, jinsi Mungu mwenyewe alivyokuwa mwanadamu kamili bila kuacha kuwa Mungu kikamilifu - kwamba Mungu, katika Uungu wake wote, alijiunganisha mwenyewe na uanadamu wote. Historia ya kanisa imeuita “muungano wa hypostatic,” muunganisho wa asili mbili tofauti katika mtu mmoja asiyegawanyika (“hypostatic” ni neno la dhana tu linalomaanisha “nafsi”). Yesu ni Mungu kamili na mwanadamu kamili katika mtu mmoja wa ajabu.


Na muungano huu wa Mungu na mwanadamu katika Yesu ndio unaowezesha muungano wetu wenyewe na Uungu kupitia kwake. Lakini siri kuu zaidi sio jinsi tunavyounganishwa na Mungu kwa imani (kupitia neema tupu na kazi ya Roho), bali jinsi Mungu alivyojiunganisha kwetu katika nafsi moja ya Kristo.


"Muungano ni mkamilifu sana," asema DA Carson , "kwamba ingawa ana asili mbili, yeye ni mtu mmoja tu." Ni karibu na kuwa nzuri mno kuwa kweli. Na kwa hivyo, "Yesu kiukweli anabeba pamoja nasi kila kitu kinacho maanisha kuwa mwanadamu," anaongeza Russell Moore .


Kweli Yeye Ni Mwanadamu

Unapomuuliza Moore kuhusu utu wa Kristo, ni Waebrania 2:11–14 , kuhusu ubinadamu wa Yesu, inayoibuka akilini.


"Ubinadamu wa Yesu mara nyingi ni jambo gumu kuelewa kwa wanadhehebu la kiinjili [evangelical]," asema. Sisi ni wepesi kuukumbatia Uungu wa Kristo, angalau wale walio kiorthodoksi kati yetu. Tumejifunza tangu siku ya kwanza kwamba Yesu ni Mungu. “Tunauelewa Uungu wake. Lakini pia, alikuwa mtu halisi na wa kweli kabisa, na bado ni mtu halisi na wa kweli."


Moore anarudia “fensi nne” zinazotoka kwenye mabaraza ya kanisa la awali na kutulinda dhidi ya makosa inapokuja kwenye fumbo hili kuu la Krismasi katika nafsi ya Kristo: Yeye ni

  1. Mungu kamili,

  2. mwanadamu kamili,

  3. kama mtu mmoja ndani ya

  4. asili mbili.


“Alijifanya Si Kitu"

Ugumu mmoja katika hili kwa akili ya mwanadamu ni kwamba tuna mwelekeo wa kuufikiria uungu na ubinadamu kama mambo mawili yasiohusiana.  Tunaweza kukisia, Ikiwa “alikuwa mwanadamu,” lazima awe ameacha kwa maana fulani, kuwa Mungu. Kisha tunakutana na andiko kama Wafilipi 2:7, kwamba “alijifanya kuwa hana utukufu,” na kuuliza, Je, alijiondolea sifa za umungu?


Carson anajibu, usemi huu hauongelei kile alichojivua; ni njia ya kimaandiko ya kusema akawa mtu asiyefaa kitu, alijinyenyekeza kabisa, si tu kuwa binadamu, bali kwenda mpaka kwenye fedheha na aibu na mateso ya msalaba. . . . Inazungumzia hali ya kushangaza, isiyo na usawa, isiyofikirika, isiyoelezeka, ya kujidhalilisha kwa kuwa binadamu na kisha kwenda mbali zaidi sio tu kuwa mtumwa, bali mtumwa anayekufa msalabani.


Fumbo Linalofichua: Masomo Matatu

Umwilisho unabaki kuwa fumbo kuu, lakini Maandiko hayaachi kila kitu kuwa kigumu. Kutoka kwenye mahojiano yetu ya dakika 17 na Carson na dakika 14 na Moore, kuna masomo matatu muhimu ambayo mafundisho haya ya ajabu yanafichua.


1. Uungu na ubinadamu havitengani.

"Asili hizi mbili hazikinzani," asema Carson. “Yeye ni mwanadamu kikweli, katika njia zote, na Mungu wa kweli, kwa njia zote, katika asili mbili zinazodumisha utofauti wao, lakini wakati huo huo, tunasisitiza kwamba asili hizi zimeunganishwa sana hivi kwamba yeye ni mtu mmoja tu. . . . Ni lugha kama hiyo ambayo inahitajika ili kuhifadhi sauti zote tofauti zinazochangia Agano Jipya ili kueleza vya kutosha, kwa ufupi, yale ambayo Biblia husema kuhusu Yesu kuwa Mungu-mwanadamu.”


Na somo hili kuhusu nafsi ya Kristo, kwamba Uungu kamili na ubinadamu kamili vinakamilishana, linatoa taswira ya mambo mengine yanayopinda akili, yenye halisi nyingi pia, kama vile uandishi wa kimungu na wa kibinadamu wa Maandiko, na mvutano wa kiungu-kibinadamu kati ya ukuu wa Mungu na wajibu wa mwanadamu.


2. Ubinadamu ni muhimu, kama vile maisha yetu duni.

Moore anaitaja miongo mitatu ya Yesu akiwa “kibarua katika mahali pasipo-julikana kabisa.” Mwaka baada ya mwaka katika maisha yake ya utulivu, kabla ya kuanza "huduma ya hadhara," hutumika kama uthibitisho wa ajabu na utakaso wa maisha yetu binafsi ya kila siku.


Na kufanyika kwake mwanadamu pia kunaonyesha thamani ya ajabu, upendeleo, na adhama ya mwanadamu kama viumbe wa juu wa Mungu. Hata juu ya malaika. Haya “mambo ambayo sasa yametangazwa kwetu kupitia wale waliohubiri habari njema” ni “mambo ambayo malaika hutamani kuyatazama” (1 Petro 1:12). Sio malaika ambaye sasa ameketi kwenye kiti cha enzi cha ulimwengu, bali ni mwanadamu (Waebrania 2:9). Ni neema iliyoje ya ajabu kwamba Yesu “haoni haya kutuita sisi ndugu zake” (Waebrania 2:11).


"Mungu amejiunga na sisi milele, amejitambulisha nasi milele." -rusell moore

3. Yesu ndiye kiungo kikuu cha maombi na ibada.

Kwa kuwa mwanadamu, amekuwa sura inayoonekana ya Mungu asiyeonekana kwa ajili yetu  (Wakolosai 1:15). Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Baba yake (Waebrania 1:3). “Nuru yetu ya ujuzi wa utukufu wa Mungu” inakuja “katika uso wa Yesu Kristo” (2 Wakorintho 4:6), naye ndiye “taa” ya umoja itakayotoa nuru ya utukufu wa Mungu katika uumbaji mpya usio na haja ya jua au mwezi (Ufunuo 21:23).


Na hivyo, asema Moore, kuomba “katika jina la Yesu” si maneno ya kichawi. “Yesu ndiye mwanadamu pekee aliye na haki ya kumkaribia Mungu.” Ni nani awezaye kupanda mlima wa Bwana? ni swali la Zaburi 24, na jibu la mwisho ni kwamba Yesu ndiye pekee anayetimiza maono kikamilifu, na ndani yake tu tunaweza kupaa.


Siri kuu ya Krismasi ni ufunuo wake mkuu pia. “Mungu amejiunga nasi milele,” asema Moore. "Mungu amejitambulisha nasi milele."

Комментарии


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page