Kumkumbatia Yesu
- Dalvin Mwamakula
- Mar 31
- 3 min read

Huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake. Na amri zake sio mzigo mzito. Kwa maana kila mtu aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, imani yetu. (1 Yohana 5:3-4)
Tazama: Kumpenda Mungu sio kushika amri zake pekee. Ni kuwa na aina ya moyo kwa ajili ya Mungu ambao unamaanisha kwamba kushika amri sio mzigo. Ndivyo asemavyo Yohana. Lakini kisha anaweka ukweli huo kwenye misingi ya kuzaliwa upya na imani, badala ya upendo. Anasema, bila mapumziko, “Kwa maana”— yaani, hii ndiyo sababu amri za Mungu sio mzigo mzito: “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Kwa hiyo, kuzaliwa upya ndiko kunakoshinda vizuizi vya kidunia vya kushika amri za Mungu bila kuelemewa.
Na hatimaye anaongeza, "Na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu”— imani yetu." Kwa hiyo, kuzaliwa upya kunashinda vizuizi vya kilimwengu vya kushika amri bila mzigo, kwa sababu kuzaliwa upya huleta imani. Kwa hiyo, muujiza wa kuzaliwa upya huleta imani, ambayo inakumbatia yote ambayo Mungu yuko kwetu katika Kristo kama yenye kutosheleza kabisa, ambayo hufanya utii kwa Mungu kuwa wa kupendeza zaidi kuliko majaribu ya dunia. Na hiyo ndiyo maana ya kumpenda Mungu.
Mchungaji na mwanatheolojia Jonathan Edwards wa karne ya kumi na nane alishindana na andiko hili na kuhitimisha, “Imani inayookoa inamaanisha . . . upendo. . . . Upendo wetu kwa Mungu hutuwezesha kushinda matatizo ambayo huambatana na kutii amri za Mungu—ambayo huonyesha kwamba upendo ndilo jambo kuu katika imani ya wokovu, uhai na nguvu zake, ambazo huleta matokeo makubwa.”
Imani ya kweli inamkumbatia Kristo kwa njia zote ambazo Maandiko yanamshikilia kwa wenye dhambi maskini.
Nadhani Edwards yuko sahihi na kwamba maandiko mengi katika Biblia yanaunga mkono anachosema.
Njia nyingine ya kusema ni kwamba imani katika Kristo sio tu kukubali kile ambacho Mungu ni kwa ajili yetu, lakini pia kukumbatia yote aliyo kwa ajili yetu katika Kristo. "Imani ya kweli inamkumbatia Kristo kwa njia zozote ambazo Maandiko yanamshikilia kwa wenye dhambi maskini" - hiyo ni nukuu nyingine kutoka kwa Edwards. "Kukumbatia" hii ni aina moja ya upendo kwa Kristo - aina inayomthamini zaidi ya vitu vyote.
Kwa hiyo, hakuna kukinzana kati ya 1 Yohana 5:3, kwa upande mmoja, ambayo inasema kwamba upendo wetu kwa Mungu hutuwezesha kushika amri zake, na mstari wa 4, kwa upande mwingine, unaosema kwamba imani yetu inashinda vikwazo vya ulimwengu vinavyotuzuia tusizitii amri za Mungu. Upendo kwa Mungu na Kristo unatokana na imani.
Kisha Yohana anafafanua imani inayotii kuwa “ile inayoamini Yesu alivyo Mwana wa Mungu” (1 Yohana 5:5). Imani hii ni "kumkumbatia" Yesu wa sasa kama mtu mtukufu wa kimungu ambaye ni: Mwana wa Mungu. Si kukubaliana tu na ukweli kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, kwa sababu mapepo wanakubali jambo hilo pia. “Wakapiga kelele, ‘Una nini nasi, Ee Mwana wa Mungu? Je! umekuja kututesa kabla ya wakati wake?’” (Mathayo 8:29). Kuamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kunamaanisha "kukumbatia" umuhimu wa ukweli huo - thamani ya ukweli huo. Inamaanisha kuridhika na Kristo kama Mwana wa Mungu na yote aliyo Mungu kwa ajili yetu ndani yake.
“Mwana wa Mungu” inamaanisha kwamba Yesu ndiye mtu mkuu zaidi katika ulimwengu wote mzima pamoja na Baba yake. Kwahiyo, yote aliyofundisha ni kweli, na yote aliyoahidi yatasimama imara, na ukuu wake wote wa kuridhisha nafsi hautabadilika kamwe.
Kuamini kwamba yeye ni Mwana wa Mungu, kwa hiyo, kunajumuisha kuweka uhakika juu ya haya yote, na kuridhika nayo.
Comments