Kushangazwa na Ufufuo
- Dalvin Mwamakula
- Jan 27
- 2 min read

Huu ndiyo waraka wa pili ninayowaandikia, wapenzi. Katika zote mbili ninachochea nia zenu safi kwa njia ya kuwakumbusha. (2 Petro 3:1)
Pasaka inapokaribia, hebu tuamshe shukrani na shangwe na kustaajabishwa kwa nini ufufuo wa Yesu unavyomaanisha kwetu. Laana ya asili yetu iliyoanguka ni kwamba kile ambacho wakati fulani kilitufurahisha kinaanza kuwa cha kawaida. Ukweli haujabadilika. Sisi tumebadilika.
Hii ndiyo sababu ya uwepo wa Biblia. Petro anasema kuhusu barua zake mbili kwamba zimeandikwa ili ‘kuchochea’ au ‘kuamsha’ kupitia “ukumbusho.”
Kwa hiyo, tuamshe akili zetu kwa njia ya ukumbusho.
Mungu amefanya nini kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu? Hapa kuna baadhi ya majibu ya kibiblia.
Laana ya asili yetu ni kwamba tunachokifurahia huanza kuonekana kama kitu cha kawaida. Ukweli haujabadilika; sisi tumebadilika.
Kwa sababu ya ufufuo wa Yesu, tunazaliwa mara ya pili kwa tumaini lililo hai.
1 Petro 1:3: “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tuwe na tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo kutoka kwa wafu.”
Kwa sababu ya ufufuo wa Yesu, sasa anao utukufu ambao kwa ajili yake tuliumbwa. Hatima yetu kuu ni kumuona jinsi alivyo.
1 Petro 1:21: “Mungu . . . alimfufua kutoka kwa wafu na kumpa utukufu.”
Yohana 17:5 , 24: “Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe kwa utukufu niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. . . . Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami nilipo, wauone utukufu wangu ulionipa kwa sababu ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.”
Bwana Yesu mfufuka mwenyewe aiamshe na kuchochea akili yako ya kweli kwa kina kipya cha ibada na utii na furaha.
Comments