HURUMA KUU YA KABILA LAKE
Makala imeandwika na John Piper
Mwanzilishi na Mwalimu, desiringGod.org
DHAHANIA: Mwokozi wa ulimwengu, Yesu Kristo, alizaliwa kama Myahudi. Kusudi la Mungu ni lipi kuhusu Uyahudi wa Yesu? Simulizi inaturudisha nyuma mpaka kwa Ibrahimu, na hutupeleka mbele kwa jamii ya watakatifu wa kutoka kila kabila, lugha na watu na taifa. Hatimaye, Yesu alizaliwa akiwa Myahudi kuharibu kila kiburi cha utaifa kujiona kuwa ni bora kuliko wengine, na kutengeneza taifa moja jipya, lenye furaha, lenye kupenda rehema.
Kwa ajili ya makala zetu maalumu zinazoendelea zilizoandaliwa na wasomi kwa ajili ya wachungaji, viongozi, na waalimu, John Piper hututafakarisha juu ya kusudi la Mungu juu ya Uyahudi wa Yesu, Kwanini Yesu azaliwe Myahudi.
Yesu alizaliwa akiwa Myahudi sio tu ili kuwavua uwongo wa kujidai Ukristo kutoka kwa Wanazi mamboleo na KKK, lakini pia kufunga midomo ya majigambo yote ya kikabila na ya rangi, pamoja na yale ya Wayahudi. Alizaliwa Myahudi ili kuleta na kufanya kila jamaa, utaifa na lugha katika hali ya unyenyekevu ili wote wategemee rehema. Alizaliwa Myahudi ili kila kabila lipate kufurahi katika huruma, si katika viwango vya kemikali za kubadili rangi- yaani melanini; na kila tamaduni ipate kufurahi katika huruma, zaidi ya njia za kitamaduni; na kila kabila lipate kufurahi katika huruma, zaidi ya sifa za kikabila. Yesu alizaliwa Myahudi ili kuharibu kila kujisifu katika ukuu wa kikabila.
Kufikia hitimisho hili ni ngumu, ingawa kihistoria Uyahudi wa Yesu umekomesha kiburi cha kikabila, hata kiburi cha Kiyahudi. Kusema ni ngumu, hata hivyo, ni kukubaliana na Paulo tu. Mara tu anapofikia hitimisho hili, anasema, katika pumzi inayofuata, "Ah, kina cha utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! "Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!" (Warumi 11:33).
"Yesu alizaliwa Myahudi ili kuharibu na kuondoa majivuno yote katika ukuu wa kikabila. Na kutengeneza utaifa mmoja mpya, wenye furaha, na kupenda rehema."
Hilo ndio jibu la Paulo kuhusu kwanini Mungu wa dunia ajifungamanishe mwenyewe pamoja na Uyahudi kama njia ya kuwaokoa watu wa kila jamaa na lugha. Ninasema "kufungamana" si kwa sababu Mungu amenaswa au kuchanganyikiwa, bali kwa sababu uingizaji wa njia zake za kuokoa na Uyahudi ni, kwa mtazamo wetu, "zisizochunguzika." Ugumu wa kueleweka kwake kwetu huzidi uwezo wetu.
Hata hivyo, Paulo alipewa idhini na Mungu kutupaisha juu zaidi katika siri hii kuliko yeyote aliyewahi kutokea. Hakuna ambaye ameweza kuielewa kwa kina. Nakualika wewe uende pamoja nami katika siri hii angalau kwa kadiri niwezavyo kwa kutumia makala hii moja.
'Kutoka katika Utaifa Wao, Kulingana na Ubinadamu'
Yesu alizaliwa akiwa Myahudi. Yule Mwanamke Msamaria pale kisimani alimwambia Yesu, "Imekuwaje wewe, Myahudi, kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria?" (Yohana4:9). Baadaye Yesu akamwambia, "Ninyi mnaabudu msichokijua, sisi tunaabudu tukijuacho, kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi" (Yohana 4:22).
Uyahudi wa Yesu haukutokea kwa bahati mbaya kwa mtume Paulo. Akauliza, "Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara?" Alijibu, "Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wame-kabidhiwa lile Neno halisi la Mungu. " (Warumi 3:1-2). Ndipo alikamilisha orodha yake kama ifuatavyo:
Yaani, watu wa Israeli, ambao ndio wenye kule kufanywa wana, ule utukufu wa Mungu, yale maagano, kule kupokea sheria, ibada ya kwenye Hekalu na zile ahadi. Wao ni wa uzao wa mababa wakuu wa kwanza, ambao kutoka kwao Kristo alikuja kwa jinsi ya mwili kama mwanadamu, yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, mwenye kuhimidiwa milele! Amina. (Warumi 9:4-5)
Jiwe la msingi la upendeleo wa Wayahudi ni hili: "Kutoka katika uzao wao, kwa jinsi ya mwili, alitoka Kristo." Yesu alizaliwa akiwa Myahudi. Na kuweka wazi upendeleo huu katika ulimwengu, yeye ni Mungu aliye fanyika mwili - "Mungu aliye juu ya yote, mwenye kuhimidiwa milele." Upendeleo kiwango cha juu zaidi kwa Waisraeli ni kuwa Mwana wa Mungu alizaliwa kati yao.
"Kila kinywa kimezuiwa. Kujivuna kwa kila kabila kumeondolewa. Wote wameingizwa katika kutokutii."
Kwa hiyo, Yesu alizaliwa akiwa Myahudi. Na hili halikutokea kwa bahati, bali lilikuwa ndiyo kiini kikuu cha upendeleo wa Kiyahudi kati ya mataifa yote. Na Paulo hakufanya kuwa siri, kana kwamba ni jambo la kustaajabisha, lakini aliiweka juu kama bendera kwa ajili ya kila Myahudi na kila taifa waweze kuiona.
Swali ni kwanini. Si tu kwanini katika mtazamo wa, Hili lilitokea wapi? Lakini pia kwanini katika mtazamo wa, hili linatuelekezea wapi? Kusudi la Mungu ni lipi kuhusu Uyahudi wa Yesu? Na ikiwa hauna maana kwa wakati uliopo, kwasababu Yesu kwa wakati huu ni mwokozi wa watu wote, je, ni kwanini Paulo hamwachi mbwa aliyelala aendelee kulala?
Kwanini - Hili limetokea wapi?
Mungu alifungamana pamoja na wanadamu kama mwenye asili ya kiyahudi kwasababu miaka elfu mbili mwanzoni inajihusisha mwenyewe na Ibrahimu, aliye baba wa Wayahudi. "Wewe ni Bwana, Mungu ambaye uliye mchagua Abramu na ukamleta kutoka Uru wa Ukaldayo nawe ukampa jina Ibrahimu" (Nehemia 9:7). Kutoka hapo, Wayahudi walifanyika kuwa watu wa agano waliopendelewa na Mungu. "Ni ninyi tu nilio wajua katika jamaa zote zilizopo duniani." (Amosi 3:2). "Bwana Mungu wako, amewachagua ninyi kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi" (kumbukumbu la Torati 7:6).
Kwa hakika, Mungu alikuwa na mtazamo huu, kutoka mwanzo kabisa, kwamba kupitia Ibrahimu na wazao wake Mungu angeliyabariki mataifa yote. "Nitawabariki wale wanaokubariki, na yule anaye-kudharau nitamlaani, na katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa" (Mwanzo 12:2-3). Lakini upendeleo wa kipekee kwa Waisraeli uliendelea kubakia.
Kwa miaka elfu mbili, Mungu aliweka kipaumbele katika shughuli zake za kuokoa ulimwengu juu ya Waisraeli, na sio kwa mataifa. "Katika vizazi vilivyopita aliwaruhusu mataifa yote kuenenda katika njia zao wenyewe" (Matendo 14:16). "Tena, Bwana aliwafurahia baba zako na kuwapenda, akawachagua wazao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo" (Mambo ya Walawi 10:15). Msamaha wa dhambi ulitolewa kwa Wayahudi kupitia kivuli cha damu ya Kristo kwenye sadaka za dhabihu (Mambo ya Walawi 4:20, Warumi 3:25). Na ahadi ilitolewa kwa Wayahudi kuwa Masia angelitokana na watu hawa (Isaya 9: 6 -7). "Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake, Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho." (Luka 1:32-33).
"Yesu alizaliwa myahudi ili kuharibu kila kujivuna katika ubora wa kikabila au utaifa."
Hii ndio sababu kwanini Yesu alizaliwa Myahudi. Mungu aliwachagua Wayahudi kuwa "tunu na watu miliki yake hasa" (Kumbukumbu la Torati 14:2). Alijikita kwa kazi yake ya ukombozi kupitia wao kwa miaka elfu mbili- sio kwa Wachina, si Waafrika, na si kwa Wajerumani. Hata "ulipotimia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria" - ikiwa na maana kuwa, alizaliwa akiwa Myahudi (Wagalatia 4:4).
Kwanini - Hii inaelekea wapi?
Lakini kujibu swali la kwa nini kuhusu zamani tu huongeza nguvu ya swali la kwanini kuhusu siku zijazo. Kusudi la Mungu kujifunga na Israeli kwa agano na Masihi Myahudi kwa kujifanya mwili ni lipi? Hii yote ilikuwa inaelekea wapi? Na kwa nini kufanya hivyo?
Kwa uwazi, maisha na kifo na kufufuka kwa Masihi Myahudi huyu ilikuwa inaelekea kuokoa Mataifa, taifa. Katika maisha yake, Yesu alisema, "Wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi na kukaa mezani pamoja na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni, wakati wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje" (Mathayo 8:11-12). Alisema kwa viongozi Wayahudi, "Ufalme wa Mungu uta chukuliwa kutoka kwenu na kutolewa kwa watu wanao zalisha matunda yake" (Mathayo 21:43). Na alimaliza huduma yake kwa amri ya "kufanya wanafunzi wa mataifa yote" (Mathayo 28:19).
Lakini wokovu ulikuwa bado "kutoka kwa Wayahudi" (Yohana 4:22). Paulo anaelezea jinsi gani. Wakati Israeli walipomkataa Yesu kama Masihi, walikuwa kama matawi ya asili yaliyo vunjwa kutoka kwenye mti wa agano na Ibrahimu. Wakati watu wa mataifa waliamini katika Masihi Yesu, walikuwa kama matawi yasiyo ya asili yaliyo pandikizwa katika Agano la Kiyahudi.
Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka shina la mzeituni, basi usijivune juu ya hayo matawi. Kama ukijivuna, kumbuka jambo hili: si wewe unayelishikilia shina, bali ni shina linalokushikilia wewe. (Warumi 11:17-18)
Mizizi inakusaidia! Hii inamaanisha ahadi ya Mungu kwa Israeli ndio sababu wewe unaokolewa, kwa sababu umeshikamana na mzizi huu.
"Hakuna wazo la watu wa Mataifa kuwa na njia moja ya wokovu, na Wayahudi njia nyingine. Kuna njia moja."
Yaani, hakuna wazo la watu wa mataifa mengine kuwa na njia moja ya wokovu, na Wayahudi nyingine. Kuna njia moja. Jiunge na Israeli ya kweli - Israeli iliyookolewa. Paul alikuwa amefanya iwe wazi kwamba "si wote ambao wanatokana na Israeli wanahesabiwa kuwa ni Israeli" (Warumi 9:6). Asili ya kiasili haimfanyi mtu kuwa sehemu ya Israeli ya kweli. Na wengi ambao hawakuwa Waisraeli wamefanywa kuwa sehemu ya Waisraeli wa kweli- "ambaye aliwaita, si kutoka katika Wayahudi pekee lakini pia kutoka katika [Mataifa.] Ni kama vile alivyosema katika Hosea, 'Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa "watu wangu'''' (Warumi 9:24-25).
Kuwa Myahudi wa kweli si swala la utaifa, bali inahusiana na kumwamini Masia: "Kwa maana mtu si Myahudi kwa vile alivyo kwa nje... Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho, wala si la sheria iliyoandikwa" (Warumi 2:28-29). Watu wa mataifa, kwa namna hii, "huwa Wayahudi."
Hivi ndivyo ahadi kwa Ibrahimu katika Mwanzo 12:3 inavyo timizwa: "Maandiko, yakiona kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, yalimhubiria Injili mapema Ibrahimu, yakisema, 'Katika wewe mataifa yote watabarikiwa'" (Wagalatia 3:8). Hivi ndivyo Ibrahimu anavyokuwa "baba wa mataifa mengi" (Mwanzo 17:5; Warumi 4:17).
"Ukombozi unatoka kwa Wayahudi" si kwa sababu Yesu alikuwa Myahudi tu, bali kwa sababu huwaokoa watu wa mataifa kwa kuwafanya washiriki kamili wa urithi wa Kiyahudi. Kupitia damu ya Kristo, "sisi wote [Wayahudi na Wamataifa] tumekubaliwa kupitia Roho mmoja kwa Baba. Basi tangu sasa ninyi [wa mataifa] si wageni wala wapitaji tena, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu". ( Waefeso2:18-19). Mataifa "wageni" wana fanyika raia wa kweli kikamilifu, wanafamilia wa Kiyahudi waliookolewa. "Ninyi [Wayahudi na Wa mataifa] ni uzao wa Ibrahimu, warithi sawa na ahadi." (Wagalatia 3:29).
'Waisraeli Wote Wataokolewa'
Baadhi ya watu hudhani kuwa kuingizwa huku kwa Watu wa Mataifa katika urithi wa Wayahudi ni hatua ya mwisho ya Mungu kushughulika na wazawa wa Israeli. Sio Hivyo. Paulo anafundisha kwamba wakati "idadi ya watu wa Mataifa watakoingia itimie," basi "Israeli wote wataokolewa" (Warumi 11:25-26). Hii inahusu taifa la kikabila kwa ujumla, likigeuzwa kuwa wakristo wakati ujao - baada ya "ukamilifu wa watu wa mataifa" kukusanywa.
Wengine wanasema "Israeli wote" hapa haimaanishi taifa la kikabila bali idadi kamili ya wateule, Wayahudi na watu wa mataifa mengine. Kuna angalau sababu tano za kushawishi kwanini hiyo haifanyi kazi. Nitataja mbili.
"Hakuna taifa lolote duniani lililostahili baraka za Mungu. Wote walistahili kuangamizwa."
Kwanza, ni jambo lisilowezekana sana kwamba, kwa maneno ya Kigiriki kumi na moja tu kati yao, maana ya "Israeli" ingebadilika kutoka "taifa la kikabila" hadi "Wayahudi na watu wa Mataifa waliochaguliwa" (Warumi 11:25-26). Matumizi ya kwanza, karibu wote wanakubaliana, yanahusu Israeli ya kikabila. Bila shaka, hivyo basi, ya pili pia itakuwa: "Ugumu wa moyo umewapata Waisraeli... Waisraeli wote wataokolewa." Hivyo "Waisraeli wote" ni taifa la kikabila ambalo awali lilikuwa limefanya shingo yake kuwa ngumu kwa sehemu. Siku moja hao watu wataokolewa.
Kwa upili, kulinganisha kati ya sehemu mbili za Warumi 11:28 inadokeza "Israeli yote" kama taifa la kikabila. Nusu ya kwanza ya aya ya 28 inasema, "Kuhusu injili, wao [watu wa kabila la Israeli] ni maadui" wa Mungu. Nusu ya pili ya aya inasema, "Lakini kuhusu uchaguzi, wao [hao watu wa kabila moja ambao ni maadui] wanapendwa kwa ajili ya mababu zao." Lengo la aya hii ni kuonyesha kwamba ingawa taifa la Israeli sasa ni watu wanao vunja agano na wasioamini, hali hiyo itabadilika. Watu ambao ni maadui sasa wataokoka baadaye kwa sababu ya uchaguzi na upendo. (Tazama pia mifano katika Warumi 11:12 na 15.)
Kwa Nini Aliifanya Hivi?
Sasa tuko katika nafasi ya kurudi nyuma na kuuliza, Kwa nini Mungu aliamua kuokoa watu wake kutoka mataifa yote, pamoja na Wayahudi, kwa njia hii ya kuzunguka?
Niruhusu niweze kufupisha njia isiyo ya moja kwa moja ya Mungu:
Watu wote walitumbukia katika dhambi na uharibifu wakati Adamu na Hawa walipo kataa wema wa Mungu kwa ajili ya hekima yao wenyewe (Mwanzo 3:6; Warumi 5:12). Kwa kuwa aina mbalimbali za watu wa kabila zilitoka katika Mwanzo 10 na 11, wanachama wao binafsi wote walikuwa "watoto wa ghadhabu" (Waefeso 2:3). Hakuna taifa lolote duniani lililostahili baraka za Mungu. Wote walistahili kuangamizwa.
2. Kama Mungu alianzisha mpango wa ukombozi kwa binadamu, alichagua Israeli kuwa kitovu kikuu cha kazi yake ya kuokoa kwa miaka elfu mbili (Kumbukumbu la Torati 7:6; Amosi 3:2). Uchaguzi huu wa Israeli kutoka kwa mataifa yote haukuwa kutokana na sifa yoyote katika Israeli ambayo iliwafanya wawe na thamani zaidi kuliko mataifa mengine. Abrahamu alikuwa mshirikina kabla ya kuitwa na Mungu (Yoshua 24:2, 14). "Je, sisi Wayahudi tuko vizuri zaidi?" Hapana, kabisa. Kwa maana tumeonyesha hapo kabla ya kwamba, Wayahudi na Wagiriki wote wako chini ya dhambi" (Warumi 3:9).
"Heshima kubwa kabisa ya watu wa Kiyahudi ni kwamba Mwana wa Mungu alizaliwa Mwisraeli."
3. Kwa miaka elfu mbili, Mungu alitoa wokovu kwa Israeli (Warumi 9:4-5) na akatabiri Masihi katika historia na Maandiko ya Kiyahudi (Luka 24:27). Jibu lao mara kwa mara lilikuwa kutoamini sana, kama vile Stefano alivyosema: "Enyi watu wenye shingo ngumu . . . mnakataa daima Roho Mtakatifu. "Kama baba zenu walivyofanya, nanyi vivyo hivyo" (Matendo ya Mitume 7:51). Au kama Paulo alivyosema, "Lakini kuhusu Israeli anasema [akimnukuu Mungu katika Isaya 65:2], Mchana kutwa nimewanyooshea watu wakaidi na wasiotii mikono yangu." (Warumi 10:21).
4. Athari ya kutokuamini kwa Wayahudi, licha ya faida kubwa, ilikuwa kuonyesha kwamba sheria, bila Mkombozi, haifanyi mtu ahesabiwe haki, bali inaleta tu ufunuo na kuongezeka kwa dhambi (Warumi 3:20; 5:20). Kupitia uzoefu huu, kinywa cha ulimwengu mzima kina nyamazishwa. Kwa maana, ikiwa Israeli, pamoja na faida zake zote, hakuweza "kufanikiwa kufikia sheria hiyo" (Warumi 9:31), mataifa mengine hayapaswi kufikiri mambo yalikaa vizuri kwa ajili yao. "Basi tunajua ya kwamba chochote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria, ili kila kinywa kinyamazishwe, na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu" (Warumi 3:19).
5. Kwa kufanywa mwili, maisha, kifo, na kufufuka kwa Masihi, ahadi kwa mababu zilithibitishwa, na rehema ilifunguliwa kwa mataifa yote. "Kristo alikuwa mtumishi kwa waliotahiriwa...ili kuthibitisha ahadi zilizotolewa kwa mababu, na ili watu wa mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema yake" (Warumi 15:8-9).
6. Ugumu uliingia kwa Israeli (Warumi 11:25; 2 Wakorintho 3:14), ukidumu hadi karne ya ishirini na moja. Itabaki "mpaka wakati ambapo idadi kamili ya watu wa mataifa imeingia" (Warumi 11:25).
7. Wakati huu - "nyakati za Mataifa" (Luka 21:24) - kutakuwa na maendeleo makubwa ya uinjilishaji kwa mataifa yote duniani. "Hii Injili ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kama ushuhuda kwa mataifa yote, na ndipo mwisho utakapokuja" (Mathayo 24:14).
8. Wakati "utimilifu wa watu wa Mataifa umekamilika... Israeli wote wataokolewa" (Warumi 11: 25-26).
9. Kristo atarudi na kuanzisha ufalme wake (Warumi 11:26).
10. Hii ni njia ya kuzunguka ambayo Mungu alipanga kuokoa watu wake kutoka kila kundi la kikabila, ikiwa ni pamoja na wongofu wa mwisho wa "Israeli wote" - kizazi kizima kilicholetwa kwa imani mwishoni mwa enzi hii. Kwa nini njia ndefu hivyo? Huu ni muhtasari wa jibu la Paulo katika Warumi 11:30-32:
Kama vile ninyi [Watu wa Mataifa] mlivyokuwa nyakati moja mkiwa hamumtii Mungu lakini sasa mmepokea rehema kwa sababu ya kutotii kwao [Wayahudi], vivyo hivyo wao [Wayahudi] pia sasa wametenda kwa kutotii ili kwa rehema iliyodhihirishwa kwenu [Watu wa Mataifa] wao [Wayahudi] pia wapate rehema sasa. Kwa maana Mungu amewafunga wote [Wayahudi na watu wa mataifa] katika kutotii, ili awaonyeshe huruma wote.
Kwa kufupisha muhtasari huu, tunaweza kusema, Mataifa yaliishi kwa kutotii baada ya anguko. Basi Mungu akawachagua Waisraeli. Israeli ikaishi kwa kutotii licha ya faida zake zote. Hivyo Mungu alifurikwa na huruma kwa mataifa ya watu wasio Wayahudi. Hii rehema kwa mataifa itasababisha rehema kubwa katika wongofu wa Israeli.Hivyo, watu wote wanategemea kabisa huruma, si wadhifu wala sifa.
Hii ni ngumu kuelewa. Ni ajabu. Na ni ya kimzunguko. Kwa kiwango kikubwa hivi kwamba kitu kinachofuata kutoka kinywani mwa Paulo ni hiki: "Ah, kina cha utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! "Tazama jinsi Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!" (Warumi 11:33).
Lengo la Mwisho: Kila Watu Wanyenyekee na Kutumainia Rehema
Je, ni nini lengo la mwisho la wokovu wa mzunguko namna hii? Paulo anasema hivi: "Mungu amewaita wote [Wayahudi na watu wa mataifa mengine] katika kutotii, ili awaonyeshe huruma wote" (Warumi 11:32). Paul alikuwa amesema tayari kwamba lengo lilikuwa "ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwajibike mbele za Mungu" (Warumi 3:19). Hilo ni lengo hasi. Kila kundi la kikabila linyenyekee kwa sababu ya uasi wao.
"Ahadi ya Mungu kwa Israeli ndiyo sababu umesalimika, kwa sababu umeshikamana na mizizi hii."
Wayahudi wana nyenyekea kwa sababu, licha ya faida zao zote, wao ni kama matawi yaliyovunjika, na watu wa Mataifa wanachukua mahali pao katika agano la Ibrahimu kwa imani pekee (Warumi 11:19; 9:30–31). Watu wa mataifa wananyenyekeshwa kwa sababu wanategemea imani pekee (Warumi 11:20) na kwa sababu ni mizizi ya Kiyahudi inayowaunga mkono, siyo kinyume chake (Warumi 11:18). Lazima uwe "Myahudi" ili upate kuokolewa (Wagalatia 3:7). Lakini hakuna Myahudi anaye okolewa kwa kuwa Myahudi kikabila. Kwa maana si kila Mwisraeli ambaye ni wa uzao utokanao na Israeli ni Mwisraeli halisi. (Warumi 9:6) "Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahamu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahamu watoto kutoka kwa mawe haya. " (Mathayo 3:9).
Kila kinywa kimefungwa. Kujivuna kwa kila kabila kumeondolewa. Wote wamepewa uasi. Kila mmoja amalazimishwa kumeza kiburi chake. Watu wa mataifa lazima wawe Wayahudi (Wanazi na KKK pia) ili waokolewe. Na Wayahudi lazima waache kutegemea Uyahudi na kujiunga na Mataifa katika kutegemea huruma.
Kabila Moja Linalo Tegemea na Kuthamini Huruma
Yesu alizaliwa Myahudi - na kila sehemu nyingine ya hekima ya Mungu "isiyoweza kutafutika" na "isiyoweza kueleweka" ya ilitumika - ili kufikia lengo hili. Kufunga mdomo wa kujisifu kwa kabila na rangi zote, ikiwa ni pamoja na Wayahudi, na kuwaleta kila kabila na rangi kwenye utegemezi wa unyenyekevu kwa rehema.
Yesu alizaliwa Myahudi ili kila kabila lipate kufurahi katika huruma, si katika viwango vya melanini; na kila kabila lipate kufurahi katika huruma, zaidi ya njia za kitamaduni; na kila kabila lipate kufurahi katika huruma, zaidi ya sifa za kikabila. Yesu alizaliwa Myahudi ili kuharibu kila kujisifu katika ukuu wa kikabila. Na kuunda kizazi kipya, chenye furaha, upendo wa huruma.
Kommentare