top of page

Lengo Kuu: Ndoa Inayoishi kwa Utukufu wa Mungu


Makala imeandwika na John Piper

Mwanzilishi na Mwalimu, desiringGod.org


Mada yangu kwa sura hii ni "Ndoa Inayoishi kwa Utukufu wa Mungu" Neno linaloamua katika mada hii ni neno "kwa". "Ndoa inayoishi kwa utukufu wa Mungu." Mada hii si: "Utukufu wa Mungu kwa ajili ya kuishi kwa ndoa." Na sio: "Ndoa inayoishi kupitia utukufu wa Mungu." Lakini: "Ndoa iliyoishi kwa utukufu wa Mungu."


Neno hili dogo linamaanisha kuwa kuna mpangilio wa kipaumbele. Kuna mpangilio wa ukuu. Na mpangilio uko wazi: Mungu ndio mkuu na ndoa sio. Mungu ndiye Ukweli wa muhimu zaidi; ndoa ni ya umuhimu mdogo — mdogo sana, mdogo mno bila kipimo. Ndoa ipo ili kuitukuza kweli na kustahili, na uzuri na ukuu wa Mungu, Mungu hayupo ili kuitukuza ndoa. Mpaka mpangilio huu uwe wazi na kuthaminiwa- mpaka uonekane na kuingia akilini - ndoa haitaonekana kuwa kama ufunuo wa utukufu wa Mungu lakini kama mshindani wa utukufu wa Mungu.


Kwa nini Ndoa Ipo

Naichukulia mada yangu, "Ndoa inayoishi kwa utukufu wa Mungu," kuwa jawabu la swali: Kwanini ndoa? Kwanini kuna ndoa? Kwanini ndoa ipo? Kwanini tunaishi kwenye ndoa? Hii inamaanisha kuwa mada yangu ni sehemu ya swali kubwa zaidi: Kwanini kitu chochote kiwepo? Kwa nini wewe upo? Kwanini kujamiiana kupo? Kwanini dunia na jua na mwezi na nyota vipo? Kwanini wanyama na mimea na bahari na milima na atomu na sayari vipo? Jawabu la maswali yote haya, ikijumuisha na kuhusu ndoa, ni: Vyote hivi vipo kwa ajili ya Mungu na utukufu wake.


Hivyo basi, hivi vyote vipo ili kutukuza ukweli, kustahili, uzuri na kuadhimisha ukuu wa Mungu. Si kama vile maikroskopu inavyo kuza, lakini kama vile darubini inavyokuza. Maikroskopu hukuza vitu kwa kuvifanya vitu vigodo vionekane vikubwa kuliko vilivyo. Darubini hukuza kwa kuvifanya vitu ambavyo visivyofikirika vionekane kama ni halisi. Maikroskopu hufanya kuonekana kwa ukubwa wa vitu mbali na uhalisia wake. Darubini hufanya kuonekana kwa ukubwa wa kitu kuelekea kwenye uhalisia wake. Nikisema kuwa vitu vyote vipo kwa ajili ya kutukuza ukweli na kustahili na uzuri na ukuu wa Mungu, Ninamaanisha Vitu vyote- na ndoa haswa- ipo ili kufanya kuonekana kwa Mungu katika akili na fahamu za watu kuelekea katika uhalisia.


Ili ndoa iwe na thamani na uzuri kulingana na mapenzi ya Mungu, ni muhimu kufundisha zaidi kuhusu Mungu kuliko kuhusu ndoa.

Mungu hachunguziki katika ukuu wake na adhama yake haitafutikani na uzuri wake haufikiriki. "Bwana ndiye mkuu, mwenye kusifiwa sana, wala ukuu wake hautambuliki" (Zaburi 145:3,). Kila kitu kilichopo kimekusudiwa kutukuza Ukweli huo. Mungu anasema kwa kupitia nabii Isaya (43:6–7), "Leteni wana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka miisho ya dunia, kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu" (msisitizo umeongezwa). Sisi tuliumbwa ili tuudhihirishe utukufu wa Mungu. Paulo anahitimisha sura kumi na moja za kwanza ya waraka wake kwa Warumi kwa kumwadhimisha na kumwinua Mungu kama chanzo na mwisho wa mambo yote: "Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele. Amina (11:36, msisitizo umeongezwa) Anafanya iwe wazi zaidi katika Wakolosai 1:16, ambapo anasema, "Kwake yeye [Kristo] vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana . . . vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake" (msisitizo umeongezwa).


Maana ya Kuumbwa kwa Ajili ya Mungu

Na ole wetu ikiwa tunadhani kwamba "kwa ajili yake" inamaanisha "kwa mahitaji yake," au "kwa manufaa yake," au "kwa ustawi wake." Paulo alifanya iwe wazi kabisa katika Matendo ya Mitume 17:25 kwamba Mungu "wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji chochote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote". Hapana, neno "kwa utukufu wake" na "kwa ajili yake" maana yake ni, "kwa kuonyesha utukufu wake," au "kwa kudhihirisha utukufu wake," au "kwa kuutukuza utukufu wake."


Tunapaswa kuacha hili litufikie kwa kina. Palikuwa na Mungu, na Mungu pekee. Ulimwengu ni uumbaji wake. Hauko pamoja na Mungu tangu milele. Ulimwengu sio Mungu. "Katika mwanzo kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu..." "Vitu vyote vilifanywa kupitia yeye" (Yohana 1:1, 3, ESV). Vitu vyote. Kila kitu ambacho si Mungu kilifanywa na Mungu. Hivyo zamani kulikuwa na Mungu pekee. Hivyo Mungu ni Ukweli kamili. Sio sisi.  Sio Ulimwengu. Sio Ndoa. Sisi ni matokeo. Ulimwengu ni wa umuhimu wa sekondari, sio wa msingi. Binadamu sio ukweli mkuu, wala thamani kuu, wala kipimo kikuu cha kilicho chema au kilicho kweli au kilicho kizuri. Mungu ndiye. Mungu ndiye kilele kikuu cha mwisho cha kipekee katika uwepo. Kila kitu kingine ni kutoka kwake na kupitia kwake na kwa ajili yake.


Huo ndio mwanzo wa kuelewa ndoa. Ikiwa tutakosea hili, kila kitu kita kwenda kombo. Na ikiwa tutaelewa vizuri kabisa - kweli kabisa, akilini mwetu na mioyoni mwetu - basi ndoa itabadilishwa nayo. Ndoa itakuwa kile kilichoumbwa na Mungu kiwe — onyesho la ukweli na thamani na uzuri na ukuu wa Mungu.


Mhubiri Mungu kwa Ajili ya Ndoa

Hii inapelekea hitimisho rahisi sana - rahisi sana na bado ina athari kubwa sana. Ikiwa tunataka kuona ndoa ikichukua nafasi yake ulimwenguni na kanisani kama inavyopaswa kuwa - yaani, ikiwa tunataka ndoa itukuze ukweli na thamani na uzuri na ukuu wa Mungu - lazima tufundishe na kuhubiri kidogo kuhusu ndoa na zaidi kuhusu Mungu.


Vijana wengi leo hawana mawazo mazuri kuhusu Mungu wanapoanza mahusiano na ndoa - yeye ni nani, yeye yukoje, na anafanya nini. Duniani hakuna karibu maono yoyote ya Mungu. Hayumo hata kwenye orodha ya waalikwa. Amepuuzwa kwa urahisi na kwa kustaajabisha. Na kanisani, mtazamo wa Mungu ambao wanandoa wapya huleta kwenye uhusiano wao ni mdogo sana badala ya kuwa mkubwa, na upo pembezoni badala ya kuwa katikati, na haueleweki badala ya kuwa wazi, na hauna nguvu badala ya kuwa wenye kuamua kila kitu, na hauna msisimko badala ya kuvutia mno, kiasi kwamba wanapooana, wazo la kuishi ndoa kwa utukufu wa Mungu halina maana wala maudhui.


Kumjua na kumfurahia Mungu kuliko vitu vyote, ikiwa ni pamoja na mwenzi wako, ndio ufunguo wa kuishi ndoa kwa utukufu wa Mungu.

 Tunachomaanisha na Utukufu wa Mungu

Maana ya "utukufu wa Mungu" kwa mke au mume mdogo ambaye hatoi muda  wala fikra hata kidogo kujua utukufu wa Mungu, au utukufu wa Yesu Kristo, Mwanae mpendwa wa Mungu...


  • utukufu wa milele yake ambao hufanya akili itake kulipuka na wazo lisilokuwa na mwisho kwamba Mungu kamwe hakuwa na mwanzo, bali daima alikuwepo;

  • utukufu wa maarifa yake ambao hufanya Maktaba ya Congress ionekane kama kisanduku cha kiberiti na fizikia ya quantum kama kitabu cha darasa la kwanza;

  • utukufu wa hekima yake ambayo haijawahi na haiwezi kamwe kushauriwa na watu;

  • utukufu wa mamlaka yake juu ya mbingu na dunia na kuzimu, ambaye bila idhini yake hakuna mtu wala pepo anaweza kuhamisha hata inchi moja;

  • utukufu wa upendo wake ambao hakuna ndege anayeangukia ardhi au unywele mmoja unageuka kijivu bila yake;

  • utukufu wa neno lake linalo shikilia ulimwengu na kuweka pamoja atomi na molekyuli zote;

  • utukufu wa nguvu zake kutembea juu ya maji, kusafisha wale wenye ukoma, kuponya viwete, kufungua macho ya vipofu, kusababisha viziwi kusikia, kuzima dhoruba kwa neno, na kufufua wafu;

  • utukufu wa usafi wake usio tenda dhambi kamwe, au kuwa na mwenendo mbaya kwa sekunde mbili au mawazo mabaya;

  • utukufu wa uaminifu wake usiovunjika kamwe, kutoacha neno lake lianguke chini;

  • utukufu wa haki yake kufanya hesabu zote za maadili ulimwenguni zilizopangwa au msalabani au kuzimu;

  • utukufu wa subira yake kuvumilia upumbavu wetu kwa miongo kadhaa baada ya miongo;

  • utukufu wa utiifu wake wa kifalme, uliokuwa kama mtumwa, kuukumbatia kwa hiari uchungu mkali wa msalaba:

  • utukufu wa hasira yake ambao siku moja utasababisha watu kuomba mawe na milima yawaangukie;

  • utukufu wa neema yake ambayo inamhesabia asiye na haki kuwa mwenye haki; na

  • utukufu wa upendo wake ambao una kufa kwa ajili yetu tangu wakati tulipokuwa wenye dhambi.


Watu watawezaje kuishi maisha yao ili ndoa zao zidhihirishe ukweli, thamani, uzuri, na ukuu wa utukufu huu, wakati hawatoi nguvu au muda kujua na kuthamini utukufu huu?


Ujumbe wa Maisha Yangu na Kanisa Langu

Labda unaweza kuelewa kwa nini katika miaka ishirini iliyopita ya huduma ya uchungaji nimekuja kuona lengo la maisha yangu na lengo la kanisa letu kwa njia za msingi sana: kwamba mimi nipo — sisi tupo — kusambaza shauku ya ukuu wa Mungu katika mambo yote kwa ajili ya furaha ya watu wote. Hiyo ni tathmini yetu ya mahitaji. Mpaka kuwe shauku ya ukuu na utukufu wa Mungu mioyoni mwa watu waliookolewa, ndoa haitaishi kwa utukufu wa Mungu.


Na hapatakuwa na shauku ya ukuu na utukufu wa Mungu mioyoni mwa watu waliokolewa mpaka Mungu mwenyewe, katika utukufu wake mwingi, ajulikane. Na hata julikana katika utukufu wake wa kipekee mpaka wachungaji na walimu wazungumze kumhusu bila kuchoka na kwa kina na kwa uaminifu na kwa uwazi na kwa bidii na kwa mapenzi. Ndoa inayoishi kwa utukufu wa Mungu itakuwa tunda la makanisa yaliyotiwa nuru na utukufu wa Mungu.


Kwa hivyo nasema tena, ikiwa tunataka ndoa itukuze ukweli na thamani na uzuri na ukuu wa Mungu, tunapaswa kufundisha na kuhubiri kidogo kuhusu ndoa na zaidi kuhusu Mungu. Si kwamba tunahubiri sana kuhusu ndoa, bali kwamba tunahubiri kidogo sana kuhusu Mungu. Mungu si lengo kuu au kiini cha maisha ya watu wengi. Yeye si jua ambalo sayari zote za maisha yetu ya kila siku zinashikiliwa katika mzingo wake na kupata mahali pake sahihi, palipopangwa na Mungu. Yeye ni kama mwezi, ambao unaongezeka na kupungua, na unaweza kupita usiku kadhaa bila kumfikiria.


Kwa wengi wetu, Mungu ni wa pembeni na mambo mengi mazuri mia moja yanachukua mahali yake. Kufikiria kwamba ndoa zao zingeweza kuishi kwa utukufu wake kwa kufundisha juu ya uhusiano, wakati utukufu wa Mungu uko pembeni sana, ni kama kutarajia jicho la binadamu litukuze nyota wakati hatuangalii anga ya usiku na hatujawahi kununua darubini.


Ufunguo wa uvumilivu mkubwa katika ndoa ni kuridhika kwa hali kuu katika Mungu kuliko vitu vya kidunia.

Jinsi ya Kuishi kwa Utukufu wa Mungu Katika Ndoa

Kwa hiyo kumjua Mungu na kumfurahisha Mungu na kuthamini utukufu wa Mungu kuliko vitu vyote, ikiwa ni pamoja na mwenzi wako, ndio ufunguo wa kuishi ndoa kwa utukufu wa Mungu. Ni kweli katika ndoa, kama katika mahusiano mengine yoyote: Mungu anatukuzwa zaidi tunaporidhika zaidi ndani yake.


Huu ni ufunguo unaofungua maelfu ya milango. Kuridhika kwa hali kuu katika Mungu kuliko vitu vyote vya kidunia, ikiwa ni pamoja na mwenzi wako, afya yako na maisha yako mwenyewe (Zaburi 63:3, "upendo wako thabiti ni bora kuliko uhai") ndio chanzo cha uvumilivu mkubwa ambao bila huo waume hawawezi kupenda kama Kristo, na wake hawawezi kufuata kama bibi harusi wa Kristo, kanisa. Waefeso 5:22–25 inaweka wazi kwamba waume wanachukua mifano yao ya uongozi na upendo kutoka kwa Kristo, na wake wanachukua mifano yao ya kujisalimisha na upendo kutoka kwa uaminifu wa kanisa alililokufa kwa ajili yake. Na vitendo vyote viwili vya upendo vinavyo kamilishana - kuongoza na kujisalimisha - haviwezi kudumu kwa utukufu wa Mungu bila kuridhika zaidi katika yote ambayo Mungu ni kwetu katika Kristo.


Njia Mbili Mungu Huangaza Utukufu Wake Kupitia Ndoa

Niseme kwa namna nyingine. Kuna viwango viwili ambavyo utukufu wa Mungu unaweza kung'aa kutoka kwenye ndoa ya Kikristo:


Moja iko katika kiwango cha muundo wakati wenzi wote wanatimiza majukumu ambayo Mungu alikusudia kwao - mwanamume kama kiongozi kama Kristo, mke kama mtetezi na mfuasi wa uongozi huo. Wakati majukumu hayo yanatekelezwa, utukufu wa upendo na hekima ya Mungu katika Kristo unadhihirishwa kwa ulimwengu.


Lakini kuna kiwango kingine cha kina zaidi, kiwango cha msingi zaidi ambapo utukufu wa Mungu lazima uangaze ili majukumu haya yaendelee kudumishwa kama Mungu alivyopanga. Nguvu na msukumo wa kutekeleza kujinyima na kufa kila siku, kila mwezi, kila mwaka ambayo itahitajika katika kumpenda mke asiye kamili na kumpenda mume asiye kamili lazima itoke kwenye kuridhika kukuu katika Mungu kunakotoa matumaini, na kudumisha roho. Sidhani kwamba upendo wetu kwa wake zetu au wao kwa sisi utamtukuza Mungu mpaka utoke kwenye moyo unaomfurahia Mungu zaidi ya ndoa.


Ndoa itadumishwa kwa utukufu wa Mungu na kuundwa kwa utukufu wa Mungu pale ambapo utukufu wa Mungu ni wa thamani zaidi kwetu kuliko ndoa. Tunapoweza kusema pamoja na mtume Paulo (katika Wafilipi 3:8), "Nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitayo kiasi cha kumjua Kristo Yesu Bwana wangu" - tunapoweza kusema hivyo kuhusu ndoa - kuhusu mume au mke wetu - basi ndoa hiyo itaishi kwa utukufu wa Mungu.


Ndoa itadumishwa kwa utukufu wa Mungu na kuundwa kwa utukufu wa Mungu ikiwa utukufu wa Mungu ni wa thamani zaidi kwetu kuliko ndoa.

Ninahitimisha kwa kujaribu kusema hivi kwa njia nyingine, yaani, kwa shairi ambalo niliandika kwa ajili ya mwanangu siku ya harusi yake.


Mpende Zaidi na Mpende Kidogo

Kwa Karsten Luke Piper

Kwenye Harusi yake na Rochelle Ann Orvis

Mei 29, 1995


Mungu ambaye tumempenda, na ambaye tumekuwa tukiishi kwa ajili yake, na ambaye amekuwa mwamba wetu kwa miaka ishirini na mbili pamoja nawe, sasa anatuamuru, kwa machozi matamu, kukuruhusu uende: "Mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe, na kuwa mwili mmoja usio na aibu na huru."


Hili ni neno la Mungu leo,

Na tunafurahi kulitii.

Kwa maana Mungu amekupa mwari

Ambaye hujibu kila maombi tuliyokuwa tunalia

Kwa zaidi ya miaka ishirini, dai letu 

Kwa ajili yako, kabla hatujalijua jina lake.


Na sasa nauliza niandike

Shairi - jambo hatari, kwa kuzingatia unavyojua:

mimi ni Mhubiri kuliko mshairi au Msanii.


Ninaheshimishwa na ushujaa wako, na ninafuata.

Sijutii mipaka tamu ya mistari iliyopangwa vema katikamistari iliyopimwa.

Ni marafiki wa zamani. 

Wanapenda pale Niwaombapo wanisaidie tena

Kukusanya hisia kuwa umbo

Na kuziweka imara na joto.


Na hivyo tukakutana katika siku za hivi karibuni,

Na tukafanya mafuriko ya upendo na sifa

Na ushauri kutoka moyo wa baba 

Kutiririka ndani ya benki za sanaa.

Hapa kuna sehemu ya mto,

Mwanangu: mahubiri ya shairi.


Mada yake: Sheria mbili za upendo zishangazazo; Mafundisho katika fumbo:


Ikiwa sasa unalenga kumbariki mke wako,

Basi mpende zaidi na mpende kidogo.


Ikiwa katika miaka ijayo, kwa njia fulani ya ajabu ya Mungu,

utapata utajiri wa wakati huu,

Na bila maumivu, utatembea kwa kujiamini kando ya mke wako,

hakikisha katika afya kumpenda, kumpenda zaidi ya utajiri.


Na kama maisha yako yatafungamana na marafiki mia,

na ukawazungusha na vazi la sherehe kwa upendo wako wa dhati,

mkubwa na mdogo, hakikisha, bila kujali jinsi inavyo pasuka,

kumpenda yeye, kumpenda zaidi ya marafiki.


Na ikiwa kuna wakati ambapo unachoka, na huruma inasema, "Jifanyie upendeleo."

Njoo, uwe huru; Kumbatia faraja hizi pamoja nami."

Jua hili! Mke wako anayazidi:

Basi mpende, mpende zaidi ya urahisi.


Na wakati kitanda chako cha ndoa ni safi,

Na hakuna hata kidokezo cha kishawishi 

Kwa tamaa yoyote isipokuwa kwa mke wako,

Na kila kitu ni furaha maishani,

Siri hii hulinda yote:

Nenda mpende, mpende zaidi ya ngono.


Na ikiwa ladha yako inakuwa imeboreshwa,

Na unaguswa na kile akili

Ya mwanadamu anaweza kutengeneza, na kushangazwa na

Ufundi wake, kumbuka kwamba "kwa nini"

Ya kazi yote hii iko moyoni;

Basi mpende yeye, mpende yeye zaidi ya sanaa.


Na kama sanaa yako mwenyewe siku moja itakuwa

sanaa ambayo wakosoaji wote wanakubaliana inastahili heshima kubwa,

Na mauzo yanazidi ndoto zako uzitamanizo,

Jihadhari na hatari ya jina.

Na mpende yeye, mpende yeye zaidi ya umaarufu.


Na kama, kwa mshangao wako, si wangu,

Mungu anakuita kwa kusudi la ajabu

Kuhatarisha maisha yako kwa sababu kuu,

Wala hofu wala upendo usisitishe,

Na unapo kabili lango la kifo,

Basi mpende, mpende zaidi kuliko pumzi.


Ndiyo, mpende, mpende, zaidi ya maisha;

Ah, mpende mwanamke anayeitwa mke wako.

Nenda mpende kama bora yako kabisa duniani.

Lakini zaidi ya hapa usiende. 

Lakini, ili upendo wako usije ukawa ni uongo wa mpumbavu,

hakikisha unampenda yeye chini ya Mungu.


Si busara wala wema kumwita sanamu kwa majina matamu,

na kuanguka, kama kwa unyenyekevu, mbele ya mfano wa Mungu.

Mpende

Zaidi ya mpendwa wako bora duniani

Mungu pekee ndiye anayempa thamani.


Na atajua katika nafasi ya pili

Kwamba upendo wako mkubwa pia ni neema,

Na kwamba mapenzi yako ya juu

Yanatiririka kwa uhuru kutoka kwa kiapo

Chini ya ahadi hizi, zilizofanywa kwanza

Kwako na Mungu.


Wala hazitofifia kwa kuwa zimepandwa kando ya mto

Wa Furaha ya Mbinguni, ambayo huthamini

Na kuenzi zaidi kuliko pumzi na uhai,

Ili uweze kumpa mke wako.


Zawadi kubwa unayompa mke wako ni kumpenda

Mungu kuliko maisha yake.

Na hivyo basi nakusihi sasa kubariki:

Nenda Mpende zaidi kwa kumpenda kidogo.


Sura ya Tatu katika Building Strong Families (Crossway, 2002)

コメント


bottom of page