Kama vile mwanadamu anavyowekewa kufa mara moja tu, na baada ya kufa hukumu, vivyo hivyo Kristo, akiisha kutolewa sadaka mara moja kuzichukua dhambi za watu wengi, atatokea mara ya pili, sio kushughulikia dhambi, bali kuwaokoa wale wanaomsubiria kwa hamu. (Waebrania 9:27-28)
Kifo cha Yesu kinabeba dhambi. Huu ndio moyo wa Ukristo, na moyo wa injili, na moyo wa kazi kuu ya Mungu ya ukombozi ulimwenguni. Kristo alipokufa alibeba dhambi. Alichukua dhambi zisizo zake. Aliteseka kwa ajili ya dhambi ambazo wengine walikuwa wamefanya, ili waweze kuwa huru dhidi ya dhambi.
Hili ndilo jibu la tatizo kuu katika maisha yako, iwe unahisi kama ni tatizo kuu au la. Kuna jibu la jinsi tunavyoweza kuwa na upatanisho na Mungu licha ya kuwa wenye dhambi. Jibu ni kwamba kifo cha Kristo ni dhabihu ya “kubeba dhambi za wengi.” Alizibeba dhambi zetu na kuzichukua mpaka msalabani na akafa pale kifo ambacho tulistahili sisi kufa.
tatizo kuu maishani mwako ni upatanisho na Mungu. Kifo cha Kristo ni dhabihu ya kubeba dhambi zetu, alizibeba msalabani na kufa kifo tulichostahili.
Sasa hii ina maana gani kwa ajili ya kufa kwangu? "Nimewekewa [kwangu] kufa mara moja." Inamaanisha kuwa kifo changu si cha adhabu tena. Kifo changu si tena adhabu ya dhambi. Dhambi yangu imeondolewa. Dhambi yangu "imeondolewa" kupitia kifo cha Kristo. Kristo aliichukua adhabu.
Kwanini basi mimi nife tena? Kwa sababu Mungu anataka kifo kibaki ulimwenguni kwa sasa, hata miongoni mwa watoto wake mwenyewe, kuwa ushuhuda wa kudumu wa kutisha juu ya dhambi. Katika kufa kwetu bado tunadhihirisha athari za nje za dhambi ulimwenguni.
Lakini kifo kwa watoto wa Mungu si ghadhabu yake tena juu yao. Imekuwa ni njia yetu ya kuingia katika wokovu sio hukumu.
Mungu anaruhusu kifo kibaki ulimwenguni kama ushuhuda wa dhambi. Kwa watoto wa Mungu, kifo si ghadhabu tena, bali ni njia ya kuingia katika wokovu.
Comments