Kwa wale wampendao Mungu, vitu vyote hufanya kazi pamoja katika kuwapatia mema, wale walioitwa kwa kusudi lake. (Warumi 8:28)
Ni mara chache tunajua sababu ndogo za kuteseka kwetu, lakini Biblia hutupatia sababu kuu zenye kudumisha imani. Ni vizuri kuwa na njia ya kukumbuka baadhi ya mambo hayo ili, tunapoteseka kwa ghafla, au kupata nafasi ya kuwasaidia wengine katika taabu zao, tuweze kukumbuka baadhi ya kweli ambazo Mungu ametupa ili kutusaidia tusikate tamaa.
Hapa kuna njia moja ya kukumbuka: 2T-2K-1U (au ikiwa inasaidia, chagua tatu tu na ujaribu kuzikumbuka). Malengo makuu ya Mungu katika mateso yetu ni pamoja na:
Toba: Mateso ni wito kwetu na wengine kugeuka kutoka kutukuza kitu chochote duniani zaidi ya Mungu. Luka 13:4–5:
"Au wale kumi na wanane ambao mnara wa Siloamu uliwaangukia na kuwaua: Je, mnafikiri walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko wengine wote waliokuwa wakiishi Yerusalemu? La hasha, nawaambia; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo."
Kumtegemea: Mateso ni wito wa kumwamini Mungu na sio nyenzo za kudumisha maisha za ulimwengu huu. 2 Wakorintho 1:8–9:
Tulikuwa tumelemewa kupita uwezo wetu kiasi kwamba tulikata tamaa ya kuishi. Kwa kweli, tulihisi kwamba tulikuwa tumepokea hukumu ya kifo. Lakini hiyo ilikuwa kutufanya tusijitegemee wenyewe bali tumtegemee Mungu ambaye huwafufua wafu.
Mateso haya ya muda mfupi yanatuandalia uzito wa milele wa utukufu usio na kifani.
Uadilifu: Kuteseka ni nidhamu ya Baba yetu wa mbinguni mwenye upendo ili tushiriki uadilifu na utakatifu wake. Waebrania 12:6 , 10–11:
"Bwana humrudi yeye ampendaye, na kumwadhibu kila mwana anayempokea." . . . Anatuadhibu kwa faida yetu, ili tushiriki utakatifu wake. Kwa wakati huu nidhamu yote inaonekana kuwa chungu badala ya kupendeza, lakini baadaye huwaletea wale ambao wamefundishwa nayo tunda la amani ya haki.
Thawabu: Mateso yanatufanyia thawabu kubwa mbinguni ambayo itafidia kila hasara hapa mara elfu. 2 Wakorintho 4:17:
Mateso haya ya muda mfupi yanatuandalia uzito wa milele wa utukufu usio na kifani.
Mwishowe, Kumbusho: Mateso yanatukumbusha kwamba Mungu alimtuma Mwana wake ulimwenguni kuteseka ili mateso yetu yasiwe hukumu ya Mungu bali utakaso wake. Wafilipi 3:10:
. . . ili nimjue yeye na uweza wa ufufuo wake, na kushiriki mateso yake.
Kwa hiyo, inaeleweka kwamba moyo wa Kikristo ungelia katika mateso, “Kwa nini?” kwa kuwa hatujui sababu nyingi ndogo za kuteseka kwetu — kwa nini sasa, kwa nini kwa njia hii, kwa nini muda mrefu hivi? Lakini usiruhusu ujinga huo wa sababu ndogo kukusababishie kupuuza msaada mkubwa ambao Mungu hutoa katika neno lake kwa kutuambia makusudi yake makuu kwa ajili yetu.
"Mmesikia juu ya uthabiti wa Ayubu, na mmeona kusudi la Bwana, jinsi Bwana alivyo na huruma" (Yakobo 5:11).
Comments