top of page

Maneno ya Upepo

“Je, mnafikiri kwamba mnaweza kukemea maneno, wakati maneno ya mtu aliyekata tamaa ni upepo?” (Ayubu 6:26)


Katika huzuni na uchungu na kukata tamaa, mara nyingi watu husema mambo ambayo vinginevyo wasingesema. Wanachora uhalisia kwa rangi nyeusi zaidi kuliko watakavyouchora kesho, jua litakapochomoza. Wanaimba kwa sauti za chini, na kuzungumza kana kwamba huo ndio muziki pekee. Wanaona mawingu tu, na wanazungumza kana kwamba hakuna anga.


Wanasema, “Mungu yuko wapi?” Au: “Hakuna haja ya kuendelea.” Au: “Hakuna kitu chenye maana yoyote.” Au: “Hakuna tumaini kwaajili yangu.” Au: “Kama Mungu angekuwa mwema, hilo lisingetokea.”


Tufanye nini na maneno haya? Ayubu anasema kwamba hatuhitaji kuwakaripia. Maneno hayo ni upepo, au kihalisi “kwa ajili ya upepo.” Yatapeperushwa haraka. Kutakuwa na mabadiliko ya hali, na mtu aliyekata tamaa ataamka kutoka usiku wa giza, na kujutia maneno ya haraka.


Kutakuwa na mabadiliko ya hali, ambapo mtu aliyekata tamaa atainuka kutoka usiku wa giza, akiomboleza maneno aliyoyatamka kwa haraka.

Kwa hiyo, jambo kuu ni kwamba, tusitumie mda na nguvu zetu kukemea maneno kama hayo. Yatapeperushwa yenyewe kwenye upepo. Sio lazima kukata majani ya miti katika majira ya vuli. Ni kupoteza nguvu. Muda si mrefu yatajiangusha yenyewe.


Ah, ni jinsi gani tunavyokimbilia kumtetea Mungu, au wakati mwingine ukweli, kutoka kwa maneno ambayo ni ya upepo tu. Ikiwa tungekuwa na utambuzi, tungeweza kutofautisha maneno yenye mizizi na maneno yanayovuma na upepo.


Kuna maneno yenye mizizi katika makosa makubwa na uovu mkubwa. Lakini sio maneno yote ya kijivu hupata rangi yao kutoka kwa moyo mweusi. Baadhi yamepakwa rangi hasa na maumivu, kukata tamaa. Unachosikia sio kitu cha ndani kabisa. Kuna kitu halisi na cha giza ndani ya mahali yanapotoka. Lakini ni cha muda — kama maambukizi ya kupita — ni halisi, ni chungu, lakini si mtu wa kweli.

 

Kwa hivyo, hebu tujifunze kutambua ikiwa maneno yaliyosemwa dhidi yetu, au dhidi ya Mungu, au dhidi ya ukweli, ni kwa ajili ya upepo tu — sio kutoka katika roho, lakini kutoka kwenye kidonda. Ikiwa ni ya upepo, tungojee kimya tusikemee. Kurejesha nafsi, sio kukemea kidonda, ni lengo la upendo wetu.


Kurejesha nafsi, sio kukemea kidonda, ni lengo la upendo wetu

Comments


bottom of page