Kwa ajili hiyo tunawaombea ninyi siku zote, ili Mungu wetu awafanye ninyi kustahili wito wake, akamilishe kila nia ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu yake, ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, na ninyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo. (2 Wathesalonike 1:11-12)
Ni habari njema sana kwamba Mungu anatengeneza utukufu wake ukuzwe kupitia matumizi ya neema yake. Kwa hakika, Mungu hutukuzwa kupitia nguvu ya ghadhabu yake (Warumi 9:22), lakini mara kwa mara Agano Jipya (na Agano la Kale, kwa mfano, Isaya 30:18) inasema kwamba tunapaswa kupata neema ya Mungu ili Mungu apate utukufu.
Tafakari jinsi hii inavyofanya kazi katika maombi ya 2 Wathesalonike 1:11–12. Paulo anaomba kwamba Mungu atimize maazimio yetu mema. Vipi? Anaomba kwamba yafanywe “kwa nguvu [za Mungu].” Yaani, kwamba kungelikuwapo na "matendo ya imani." Kwanini? Ili Yesu atukuzwe ndani yetu.
Hiyo ina maana kwamba mtoaji anapata utukufu. Mungu alitupa nguvu. Mungu anapata utukufu. Tuna imani; anatoa nguvu. Tunapata msaada; anapata utukufu. Huo ndio mpango unaotufanya tuwe wanyenyekevu na wenye furaha, na unaofanya aendelee kuwa mkuu na mtukufu.
Ni habari njema sana kwamba Mungu anatengeneza utukufu wake ukuzwe kupitia matumizi ya neema yake.
Kisha Paulo anasema kwamba kutukuzwa huko kwa Kristo ni “kulingana na neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu.” Jibu la Mungu kwa maombi ya Paulo kwamba tutegemee nguvu za Mungu kufanya matendo mema ni neema. Nguvu ya Mungu ya kukuwezesha kufanya kile unachoazimia kufanya ni neema.
Hivyo ndivyo inavyofanya kazi katika Agano Jipya tena na tena. Mwamini Mungu kwa uwezeshaji wa neema, na anapata utukufu msaada unapokuja. Tunapata msaada. Anapata utukufu. Ndio maana maisha ya Kikristo, sio uongofu wa Kikristo tu, ni habari njema.
Comments