top of page

Muda Kidogo Tu

Mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu, na kukuimarisha. (1 Petro 5:10)

 

Wakati mwengine katikati ya taabu na shida za kawaida za maisha za kila siku, tunaweza kulia, “Ee Bwana, hadi lini? Siwezi kuona mbele zaidi ya maumivu ya leo. Je, kesho itakuwaje? Je, utakuwepo kwa ajili ya dhiki hiyo pia?”


Swali hili ni la muhimu sana, kwa sababu Yesu alisema, "Yeye atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokolewa" (Marko 13:13). Tunatetemeka kwa mawazo ya kuwa kati ya "wale wanaorudi nyuma na kuharibiwa" (Waebrania 10:39). Hatuchezi michezo. Mateso ni tishio la kutisha imani katika neema ya Mungu ya wakati ujao.

 

Mungu ni "Mungu wa neema yote," akijumuisha hazina isiyo na kikomo ya neema ya wakati ujao tunayoihitaji kuvumilia hadi mwisho.

Kwa hiyo, ni jambo la kustaajabisha kusikia Petro akiwaahidi Wakristo wanaoteseka na waliochoka, “Mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita mpate utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu, na kuwafanya imara” (1 Petro 5:10).

 

Hakikisho kwamba hatakawia kupitia vile tunavyoweza kustahimili, na kwamba atakomesha shida tunazoziomboleza, na kwamba atathibitisha milele kile ambacho kimeyumba kwa muda mrefu sana - uhakikisho huo unatoka kwa Mungu wa "neema zote." 


Mungu sio Mungu wa neema fulani - kama neema iliyopita. Yeye ni "Mungu wa neema yote" - ikijumuisha hazina isiyo na kikomo, isiyoisha ya neema ya wakati ujao ambayo tunahitaji kuvumilia hadi mwisho.


Imani katika neema hiyo ya wakati ujao, ikiimarishwa na kumbukumbu ya neema iliyopita, ndiyo ufunguo wa kustahimili katika njia nyembamba na ngumu iendayo uzimani.

Imani katika neema ya wakati ujao, ikiimarishwa na kumbukumbu ya neema iliyopita, ndiyo ufunguo wa kustahimili katika njia ngumu iendayo uzimani.

Comments


bottom of page