top of page

Mungu Anakujali

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read

Jinyenyekezeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue kwa wakati wake ufaao, huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. (1 Petro 5:6-7)

 

Kwanini wasiwasi kuhusu siku zijazo ni aina ya kiburi?


Jibu la Mungu lingesikika kama hivi (kufafanua Isaya 51:12):


Mimi — Bwana, Muumba wako — mimi ndiye ninayekufariji, ninayeahidi kukutunza; na wale wanaokutishia ni wanadamu tu wanaokufa. Kwa hiyo, hofu yako lazima inamaanisha kuwa huniamini — na ingawa huna uhakika kwamba rasilimali zako mwenyewe zita kutunza, bado una chagua kujitegemea kwa udhaifu, badala ya kuwa na imani katika neema yangu ya baadaye. Kwa hiyo, kutetemeka kwako kote — dhaifu kama kulivyo — kunaonyesha kiburi.


Tiba yake? Geuka kutoka kujitegemea na uanze kumtegemea Mungu, na weka imani yako katika nguvu za kutosha za ahadi ya neema yake ya baadaye.


Unaweza kuona kwamba wasiwasi ni aina ya kiburi katika 1 Petro 5:6-7. Angalia uhusiano wa kisarufi kati ya mistari hiyo.


"Nyenyekeeni . . . chini ya mkono wenye nguvu wa Mungu. . .[sasa, mstari wa 7] mkimtwika yeye fadhaa zenu zote." Mstari wa 7 si sentensi mpya. Ni kishazi tegemezi. Inaanza na kitenzi kishirikishi: "Jinyenyekezeni . . . mkimtwika yeye fadhaa zenu zote."


Hii inamaanisha kwamba kumtwika Mungu fadhaa zako ni njia ya kujinyenyekeza chini ya mkono wenye nguvu wa Mungu. Ni kama kusema, “Kula kwa adabu. . . tafuna mdomo ukiwa umefunga.” Au, “Endesha kwa uangalifu… ukiwa unatazama barabara.” Au, “Kuwa mkarimu… ukiwaalika watu nyumbani katika Siku ya Shukrani.” Au, “Nyenyekeeni… mkimtwika Mungu hofu zenu.”


Kuweka wasiwasi wetu kwa Mungu ni unyenyekevu, wasiwasi usiofaa ni aina ya kiburi kisichotaka kumtegemea Yeye aliye na hekima na nguvu zote.

Njia moja ya kujinyenyekeza ni kumtwika Mungu wasiwasi zetu zote. Hii inamaanisha kwamba kikwazo kimoja cha kuweka wasiwasi wako kwa Mungu ni kiburi. Hii inamaanisha kwamba wasiwasi usiofaa ni aina ya kiburi. Haijalishi inaonekana au inahisi dhaifu kiasi gani.


Sasa, kwa nini kuweka wasiwasi wetu kwa Bwana ni kinyume cha kiburi? Kwa sababu kiburi hakipendi kukubali kwamba kina wasiwasi wowote. Au kwamba hatuwezi kuushughulikia wenyewe. Na kama kiburi kinapaswa kukubali kwamba hofu zake haziwezi kudhibitiwa, bado hakipendi kukubali kwamba tiba inaweza kuwa kumwamini mtu mwingine ambaye ni mwenye hekima na nguvu zaidi. 


Kwa maneno mengine, kiburi ni aina ya kutoamini na hakipendi kumtumaini Mungu kwa neema yake ya baadaye. Imani, kwa upande mwingine, inakubali hitaji la msaada. Kiburi hakitakubali. Imani inamtegemea Mungu kutoa msaada. Kiburi hakitakubali. Imani inatupa wasiwasi wake kwa Mungu. Kiburi hakitakubali. 


Kwa hiyo, njia ya kupambana na kutoamini kwa kiburi ni kukubali kwa uhuru kwamba una wasiwasi, na kuthamini ahadi ya neema ya baadaye katika maneno, “Anakujali.” Kisha toa hofu zako na weka kwenye mabega yake yenye nguvu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page