top of page

Mungu Anapokuwa Kwa Ajili Yetu 100%

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jan 27
  • 2 min read

. . . ambao hapo kwanza sisi sote tuliishi kati yao katika tamaa za miili yetu, tukizifanya tamaa za mwili na nia, nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama wanadamu wengine. (Waefeso 2:3)


Ghadhabu yote ya Mungu, hukumu yote tunayostahili, ilimwagwa juu ya Yesu. Matakwa yote ya Mungu ya haki kamilifu yalitimizwa na Kristo. Wakati tunapoiona (kwa neema!) Hazina hii, na kumpokea kwa njia hii, kifo chake kinahesabiwa kama kifo chetu na hukumu yake kama hukumu yetu na haki yake kama haki yetu, na papo hapo Mungu anakuwa kwa ajili yetu 100% bila kubatilishwa milele.

 

Swali ambalo halijajibiwa ni, “Je, Biblia haifundishi kwamba katika umilele Mungu aliweka kibali chake juu yetu katika uchaguzi?”

 

Kwa maneno mengine, watu wenye kufikiria huuliza, “Je, Mungu alifanyika tu kuwa kwa ajili yetu 100% wakati wa imani na muungano na Kristo na kuhesabiwa haki? Je, hakuwa kwa ajili yetu 100% katika tendo la uchaguzi kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu?” Paulo anasema katika Waefeso 1:4–5 , “[Mungu] alituchagua katika [Yesu] kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake. Katika upendo alitangulia kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo.”


Furahia ukweli kwamba Mungu atakulinda na atakufikisha mwisho, kwani ndani ya Kristo yupo kwa ajili yako kikamilifu. 

Je, Mungu basi si 100% kwa wateule tangu milele? Jibu linategemea maana ya “100%. 

 

Kwa neno "100%" ninajaribu kuhifadhi ukweli wa kibiblia unaopatikana katika vifungu kadhaa vya Maandiko. Kwa mfano, katika Waefeso 2:3, Paulo anasema kwamba Wakristo walikuwa “watoto wa ghadhabu” kabla ya kufanywa hai katika Kristo Yesu: “Sisi sote tuliishi zamani [kati ya wana wa kutotii] katika tamaa za miili yetu, tukitenda kazi tamaa za mwili na za akili, nao kwa asili walikuwa wana wa ghadhabu, kama wanadamu wengine.”

 

Paulo anasema kwamba, kabla ya kuzaliwa upya—kabla hatujafanywa hai pamoja na Kristo—hasira ya Mungu ilikuwa juu yetu. Wateule walikuwa chini ya ghadhabu. Haya yalibadilika pale Mungu alipotuhuisha ndani ya Kristo Yesu na kutuamsha ili tuone ukweli na uzuri wa Kristo ili tukampokee kama aliyekufa kwa ajili yetu na ambaye haki yake inahesabiwa kuwa yetu kwa sababu ya muungano wetu na Yesu. Kabla haya hayajatokea kwetu, tulikuwa chini ya ghadhabu ya Mungu. Kisha, kwa sababu ya imani katika Kristo na kuungana naye, ghadhabu yote ya Mungu iliondolewa na akawa, kwa maana hiyo, 100% kwa ajili yetu.


Kupitia imani ndani ya Kristo, ghadhabu ya Mungu iliondolewa na Mungu yupo kwa ajili yetu 100%.

Kwahiyo, furahia ukweli kwamba Mungu atakulinda. Atakufikisha mwisho maana ndani ya Kristo yupo kwa ajili yako 100%. Na kwa hivyo, kufika mwisho hakumfanyi Mungu kuwa kwa ajili yako 100%. Ni athari ya ukweli kwamba yeye tayari yupo kwa ajili yako 100%.


Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page