top of page

Mungu Huwathamini Wanyonge

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read

"Mungu wa milele ni makao yako, na chini kuna mikono ya milele." (Kumbukumbu la Torati 33:27)

 

Unaweza kuwa unapitia mambo sasa hivi ambayo yanakuandaa kwa uchungu kwa ajili ya huduma ya thamani kwa Yesu na watu wake. Wakati mtu anapofikia mwisho wa uwezo wake na kuhisi hana chochote au hana msaada, anaweza kugundua kuwa ameugonga Mwamba wa Milele.

 

Nakumbuka mstari mtamu kutoka Zaburi 138:6 ambayo familia yetu ilisoma wakati wa maombi ya kifungua kinywa: “Ingawa Bwana yuko juu, anamwona mnyenyekevu.” 

 

Huwezi kuzama hadi kiwango cha chini sana cha kukatia tamaa nguvu zako mwenyewe kiasi kwamba Mungu asione na asijali. Kiukweli, yupo chini akikusubiri akudake. Kama Musa anavyosema, "Mungu wa milele ndiye makazi yako, na mikono ya milele iko chini yako" (Kumbukumbu la Torati 33:27).

 

Ndiyo, anakuona unatetemeka na kuteleza. Angeweza (na mara nyingi alifanya hivyo) kukushika kabla hujafika chini. Lakini wakati huu ana masomo mapya ya kufundisha. 

 

Ni askari waliojeruhiwa pekee wanaoweza kutoa huduma katika huduma ya upendo—maumivu yako leo yanaweza kuwa maandalizi ya huduma ya thamani kwa Yesu na watu wake.

Mwandishi wa Zaburi alisema katika Zaburi 119:71, "Ilikuwa vyema kwangu kuwa naliteswa, nipate kujifunza amri zako." Hajasema kuwa ilikuwa rahisi au ya kufurahisha au ya kupendeza. Kwa kutafakari nyuma, anasema tu, “Ilikuwa vyema kwangu.”

 

Wiki iliyopita nilikuwa ninasoma kitabu cha mhubiri mmoja wa Uskochi aitwaye James Stewart. Alisema, “Katika huduma ya upendo, ni askari waliojeruhiwa pekee wanaoweza kutoa huduma.” Ndio maana naamini baadhi yenu mnaandaliwa sasa hivi kwa ajili ya huduma ya upendo ya thamani. Kwa sababu mnajeruhiwa.

 

Usifikiri kwamba jeraha lako limekupata bila mpango wa neema ya Mungu. Kumbuka neno lake: “Tazama sasa kwamba mimi, hata mimi, ndiye, na hakuna mungu mwingine zaidi yangu . . . Najeruhi na kuponya" (Kumbukumbu la Torati 32:39).

 

Mungu akujalie neema maalum wewe unayelia chini ya mzigo fulani. Tazamia kwa hamu upole mpya wa upendo ambao Mungu anakupa hata sasa.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page