Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi. (Matendo 14:22)
Uhitaji wa nguvu ya ndani hutokea sio tu kutokana na kupungua kwa matatizo ya kila siku, lakini kutokana na mateso na taabu ambayo huja mara kwa mara. Na mateso huja.
Mateso bila shaka yanaongezwa katika moyo uliochoka katika njia ya kwenda mbinguni. Yanapokuja, moyo unaweza kuyumba-yumba na njia nyembamba inayoongoza kwenda kwenye uzima inaweza kuonekana kuwa ngumu sana. Ni ngumu vya kutosha kuwa na barabara nyembamba na milima mikali inayojaribu nguvu za gari la zamani hadi ukomo wake. Lakini tutafanya nini gari litakapoharibika?
Paulo alilia mara tatu na swali hili kwa sababu ya taabu fulani katika maisha yake. Aliomba apate nafuu kutokana na mwiba wake ndani ya mwili. Lakini neema ya Mungu haikuja kwa namna aliyoomba. Ilikuja kwa namna nyingine. Kristo alijibu, “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hukamilishwa katika udhaifu” (2 Wakorintho 12:9).
Hapa tunaona neema ikitolewa kwa namna ya uweza wa Kristo wa kutegemeza katika dhiki isiyoisha — neema moja iliyotolewa, tunaweza kusema, ndani ya mzunguko wa neema nyingine iliyokataliwa. Na Paulo alijibu kwa imani katika utoshelevu wa neema hii ya wakati ujao: “Kwa hiyo nitajisifia kwa furaha nyingi zaidi katika udhaifu, ili nguvu za Kristo zikae juu yangu” (2 Wakorintho 12:9).
Neema ya Mungu haikuja alivyotarajia. bali Kristo alijibu, “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hukamilishwa katika udhaifu.”
Mungu mara nyingi hutubariki kwa "neema iliyotolewa" katika mzunguko wa "neema iliyokataliwa."
Kwa mfano, siku yenye joto kali mnamo Julai, pampu ya maji kwenye gari letu iliacha kufanya kazi, na maili ishirini kutoka katika mji wowote tulikwama kwenye eneo la kati huko Tennessee.
Nilikuwa nimesali asubuhi hiyo kwamba gari lifanye kazi vizuri na kwamba tufike salama tulipokuwa tukienda. Sasa gari lilikuwa limeharibika. Neema ya kusafiri bila matatizo ilikuwa imekataliwa. Hakuna mtu aliyekuwa akisimama tulipokuwa tumekusanyika karibu na gari letu. Kisha mwanangu Ibrahimu (miaka kumi na moja wakati huo) akasema, “Baba, tunapaswa kuomba.” Kwa hivyo tuliinama nyuma ya gari na kumwomba Mungu kwa neema ya siku zijazo — msaada wakati wa mahitaji. Tulipotazama juu, lori lilikuwa limesimama.
Dereva alikuwa fundi makanika aliyefanya kazi umbali wa maili ishirini hivi. Alisema atakuwa tayari kwenda kuchukua vifaa na kurudi kurekebisha gari. Nilipanda naye hadi mjini na niliweza kumshirikisha injili. Tulikuwa njiani katika muda wa masaa matano hivi.
Sasa jambo la kushangaza kuhusu jibu hilo la maombi yetu ni kwamba lilikuja ndani ya duara la maombi yaliyokataliwa. Tuliomba safari isiyo na matatizo. Mungu alitupa tatizo. Lakini katikati ya neema iliyokataliwa, tulipata neema iliyotolewa. Na ninajifunza kuamini hekima ya Mungu katika kutoa neema ambayo ni bora kwangu na kwa fundi makanika asiyeamini na kwa imani ya mvulana wa miaka kumi na moja.
Hatupaswi kushangaa kwamba Mungu anatupa neema ya ajabu katikati ya mateso ambayo tulimwomba atuepushe nayo. Anajua vyema jinsi ya kugawanya neema yake kwa manufaa yetu na kwa utukufu wake.
Tuliomba safari salama, lakini Mungu alitupa tatizo, kisha akatupa neema nyingine. Ninajifunza kuamini hekima ya Mungu katika kutoa neema iliyo bora kwangu...
Comentarios