top of page

Neema Kwa Ajili ya Mwaka Mpya

Kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya kazi kwa bidii zaidi kuliko wao wote, ingawa sio mimi, bali ni neema ya Mungu iliyo pamoja nami. (1 Wakorintho 15:10)

 

Neema sio tu tabia ya Mungu ya kututendea mema wakati hatustahili. Ni nguvu halisi kutoka kwa Mungu ambayo hutenda na kufanya mambo mema kutokea ndani yetu na kwa ajili yetu.

 

Neema ya Mungu ilikuwa kazi ya Mungu ndani ya Paulo ili kumfanya Paulo afanye kazi kwa bidii: “Kwa neema ya Mungu . . . Nilifanya kazi kwa bidii kuliko yeyote kati yao.” Kwa hiyo Paulo anaposema, “Utimizeni wokovu wenu wenyewe,” anaongeza, “kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu, kutaka na kutenda kwa kulitimiza kusudi lake jema” (Wafilipi 2:12–13). Neema ni nguvu kutoka kwa Mungu kufanya mambo mema ndani yetu na kwa ajili yetu.


Neema ni tabia ya Mungu kututendea mema tusiyostahili na nguvu kutoka kwake inayotenda mema ndani yetu na kwa ajili yetu.

 

Neema hii ni ya wakati uliopita na ni ya wakati ujao. Inatiririka kila wakati juu ya maporomoko ya maji yasiyo na kikomo ya sasa, kutoka kwenye mto usiokauka wa neema unaotujia kutoka wakati ujao, hadi kwenye hifadhi ya neema inayoendelea kuongezeka ya wakati uliopita.

Katika dakika tano zijazo, utapokea neema ya kudumu inayotiririka kwako kutoka wakati ujao, na utajikusanyia neema ya dakika tano zaidi kwenye hifadhi ya siku zilizo pita.  Mwitikio unaofaa kwa neema uliyopata hapo awali ni shukrani, na mwitikio unaofaa kwa neema uliyoahidiwa katika siku zijazo ni imani. Tunashukuru kwa neema iliyopita ya mwaka jana, na tuna uhakika wa neema ya siku zijazo kwenye mwaka mpya.


Mwitikio unaofaa kwa neema uliyopata ni shukrani, na mwitikio unaofaa kwa neema ya siku zijazo ni imani.

Kommentare


bottom of page