NI HAKIKA kama upendo wa Mungu kwa Mwana wake
- Dalvin Mwamakula
- Feb 26
- 2 min read
Updated: Mar 18

Ikiwa Mungu hakumhurumia mwana-wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye ? (Warumi 8:32)
Mungu huvua kila maumivu nguvu ya uharibifu wake. Lazima uamini hili au hautadumu, au labda hata kuishi, kama Mkristo, katika shinikizo na majaribu ya maisha ya kisasa.
Kuna maumivu mengi sana, vikwazo na kukatishwa tamaa sana, migogoro mingi na mashinikizo mengi. Sijui ningegeukia wapi, kama nisingeamini kwamba Mungu mwenyezi anachukua kila kikwazo na kila kukatishwa tamaa na kila mgogoro na kila shinikizo na kila maumivu, na kuondoa nguvu yake ya uharibifu, na kuifanya ifanye kazi kwa ajili ya kuongeza furaha yangu ndani ya Mungu.
Kuna maumivu na vikwazo maishani, lakini naamini Mungu hupunguza uharibifu wa changamoto hizi ili kuongeza furaha yangu ndani yake.
Sikiliza maneno ya kushangaza ya Paulo katika 1 Wakorintho 3:21–23, “Vitu vyote ni vyenu, iwe ni Paulo au Apolo au Kefa au ulimwengu au maisha au kifo au sasa au wakati ujao — vyote ni vyenu, nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.” Ulimwengu ni wetu. Maisha ni yetu. Kifo ni chetu. Ninachomaanisha ni kwamba: Mungu anatawala kwa ukuu kwa niaba ya wateule wake kiasi kwamba kila kitu kinachotukabili katika maisha ya utii na huduma kita shindwa na mkono wenye nguvu wa Mungu na kufanywa mtumishi wa utakatifu wetu na furaha yetu ya milele katika Mungu.
Ikiwa Mungu yuko upande wetu, na ikiwa Mungu ni Mungu, basi ni kweli kwamba hakuna kitu kinachoweza kufanikiwa dhidi yetu. Yeye ambaye hakumhurumia Mwanawe mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atatupa kwa uhakika na bure pamoja naye vitu vyote — vitu vyote — dunia, maisha, kifo, na Mungu mwenyewe.
Warumi 8:32 ni rafiki wa thamani sana. Ahadi ya neema ya Mungu ijayo ni yenye kustaajabisha mno. Lakini muhimu zaidi ni msingi wake: nimeuita huu kuwa ni mantiki ya mbinguni. Hapa ndipo mahali pa kusimama dhidi ya vikwazo vyote. Mungu hakumhurumia hata Mwana wake mwenyewe! Kwa hiyo! Kwa hiyo! Mantiki ya mbinguni! Ikiwa hivyo, je, hatazidisha zaidi kutupa sisi kila kitu ambacho Kristo alikifia ili kukipata—mambo yote, mema yote, na hata yale mabaya, yakitenda kazi pamoja kwa wema wetu!
Ni hakika kama vile uhakika kwamba alimpenda Mwana wake!
Comments