top of page

Njia Tano Ambazo Mateso Husaidia

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jan 27
  • 2 min read

Kabla sijateswa nilipotoka, lakini sasa natii neno lako. (Zaburi 119:67)

 

Mstari huu unaonyesha kwamba Mungu hutuma mateso ili kutusaidia kujifunza neno lake. Je, hilo linafanyaje kazi? Je, mateso yanatusaidiaje kujifunza na kutii neno la Mungu?


Kuna majibu yasiyohesabika, kwani kuna uzoefu usiohesabika wa rehema hii kuu. Lakini hapa kuna tano:

1.     Taabu huondoa wepesi wa maisha na kutufanya tuwe makini zaidi, ili mawazo yetu yalingane zaidi na uzito wa neno la Mungu. Na kumbuka hili: Hakuna ukurasa hata mmoja usio na uzito katika kitabu cha Mungu.


2.    Mateso hutupokonya tegemeo la kidunia na kutulazimisha kumtegemea Mungu zaidi, jambo ambalo hutufanya tuwe karibu zaidi na lengo la neno lake. Maana kusudi la neno hili ni kwamba tumtumaini Mungu na kumwamini. “Yote yaliyoandikwa zamani yaliandikwa kwa ajili ya kutufundisha, ili kwa uvumilivu na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini” (Warumi 15:4). “Haya [mambo] yameandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu” (Yohana 20:31).


Mateso hutulazimisha kumtegemea Mungu zaidi, Hutufanya tuwe karibu na lengo la neno lake, huku yakifisha tamaa za kimwili na kutufanya tupokee neno lake la kiroho.

3.    Mateso hutufanya tutafute Maandiko kwa bidii zaidi kwa usaidizi, badala ya kuyachukulia kama sehemu ya pembezoni mwa maisha. “Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” (Yeremia 29:13).


4.    Mateso hutuleta katika ushirikiano wa mateso ya Kristo, ili tushirikiane naye kwa ukaribu zaidi na kuuona ulimwengu kwa urahisi zaidi kupitia macho yake. Shauku kuu ya moyo wa Paulo ilikuwa “nipate kumjua yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na kushiriki mateso yake, nifanane naye katika kufa kwake” (Wafilipi 3:10).


5.    Mateso hufisha tamaa za kimwili zenye udanganyifu na zenye kukengeusha, na hivyo hutuleta katika hali ya kiroho zaidi na kutufanya tulipokee neno la kiroho la Mungu. “Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili, jivikeni silaha ya nia iyo hiyo; kwa maana kila aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi” (1 Petro 4:1). Mateso yana athari kubwa ya kuua dhambi. Na tunapokuwa wasafi zaidi, ndivyo tunavyomwona Mungu kwa uwazi zaidi (Mathayo 5:8).


Roho Mtakatifu na atujalie neema tusione ugumu katika mafundisho ya Mungu kupitia maumivu.


Taabu hutufanya tutafute Maandiko kwa bidii, tukilinganisha mawazo yetu na neno la Mungu, na kuuona ulimwengu kwa macho yake.

Comentários


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page