top of page

Riziki ya Lincoln

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jan 27
  • 2 min read

Ee, kina cha utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Jinsi hukumu zake zisivyotafutika na njia zake zisizochunguzika! (Warumi 11:33)

 

Abraham Lincoln, ambaye alizaliwa siku hii mwaka 1809, alibakia kuwa na mashaka, na wakati mwingine alikuwa mwenye wasiwasi kuhusu dini hadi umri wake wa miaka ya arobaini. Kwa hiyo, ni jambo la kushangaza zaidi jinsi mateso ya kibinafsi na ya kitaifa yalivyomvuta Lincoln katika ukweli wa Mungu, badala ya kumsukuma mbali.

 

Mnamo 1862, Lincoln alipokuwa na umri wa miaka 53, mtoto wake Willie mwenye umri wa miaka 11 alifariki. Mke wa Lincoln “alijaribu kushughulika na huzuni yake kwa kutafuta watu wa Enzi Mpya.” Lincoln alimgeukia Phineas Gurley, mchungaji wa Kanisa la Kipresbiteri la New York Avenue huko Washington. 

 

Mazungumzo kadhaa marefu yaliongoza kwenye kile ambacho Gurley alieleza kuwa “kugeuzwa imani kwa Kristo.” Lincoln alikiri kwamba "alisukumwa mara nyingi kupiga magoti kwa sababu ya imani kubwa kwamba hana pengine pa kwenda."

 

Vile vile, ukatili waliopitia askari waliokufa na waliojeruhiwa ulimshambulia kila siku. Kulikuwa na hospitali hamsini za waliojeruhiwa huko Washington. Rotunda ya Capitol ilikuwa na vitanda elfu mbili vya askari waliojeruhiwa. 

 

Ninaomba kwa ajili yenu mnaopitia hasara na huzuni kwamba itawaamsha kutegemea hekima na upendo wa Mungu katika mpango wake usioeleweka

Kwa kawaida, askari hamsini kwa siku walikufa katika hospitali hizi za muda. Haya yote yalimpeleka Lincoln ndani zaidi katika uangalizi wa Mungu. "Hatuna budi kuamini, ya kwamba yeye aliyeumba ulimwengu bado anautawala."

 

Kauli yake maarufu zaidi kuhusu majaliwa ya Mungu kuhusiana na Vita vya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa Hotuba yake ya Pili ya Uzinduzi, aliyoitoa mwezi mmoja kabla ya kuuawa. Inashangaza kwa kutomfanya Mungu kuwa mfuasi rahisi wa upande wa Muungano au wa Mshirika. Mungu ana makusudi yake mwenyewe na hasamehi dhambi kwa upande wowote.

 

Tunatumaini - tunaomba kwa bidii - kwamba janga hili kuu la vita liweze kupita upesi. . . .

 

Hata hivyo, ikiwa Mungu atapenda iendelee, hadi mali yote iliyokusanywa na kazi ya miaka mia mbili ya mtumwa bila malipo itakapozama, na hadi kila tone la damu lililotolewa kwa mjeledi, lilipwe na lingine lililotolewa kwa upanga, kama ilivyosemwa miaka elfu tatu iliyopita, hivyo bado inapaswa kusemwa, "hukumu za Bwana ni za kweli na za haki kabisa."

 

Ninaomba kwa ajili yenu nyote mnaopitia hasara, majeraha, na huzuni kubwa kwamba itawaamsha, kama ilivyokuwa kwa Lincoln, sio kukata tamaa bure, bali kutegemea zaidi hekima isiyo na mipaka na upendo wa Mungu katika mpango wake usioeleweka.


Ni jambo la kushangaza jinsi mateso ya kibinafsi na ya kitaifa yalivyomvuta Lincoln katika ukweli wa Mungu, badala ya kumsukuma mbali.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page