top of page

Saa ya Tishio Lisilo la Kawaida

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jan 27
  • 2 min read

Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa maana Roho wa utukufu na wa Mungu anakaa juu yenu. (1 Petro 4:14)


Wakristo wengi ulimwenguni leo hawajui hatari inayotishia maisha inayoletwa na kumwamini Kristo. Tumezoea kuwa huru mbali na mateso kama hayo. Inaonekana kama vile hivi ndivyo mambo ndio yanavyotakiwa kuwa. 


Kwa hivyo, mwitikio wetu wa kwanza kwa tishio kwamba mambo yanaweza kuwa vinginevyo mara nyingi ni hasira. Lakini hasira hiyo inaweza kuwa ishara kwamba tumepoteza hisia zetu za kuwa wasafiri na watu waliohamishwa (“Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na watu waliohamishwa . . . ” (1 Petro 2:11). 


Labda tumekaa sana katika ulimwengu huu. Hatuhisi kutamani nyumbani kwa Kristo kama Paulo alivyohisi: “Lakini sisi, wenyeji wetu uko mbinguni, na kutoka huko tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo” (Wafilipi 3:20).


Wengi wetu tunahitaji ukumbusho huu, “Wapenzi, msistaajabie majaribu makali yanayowajia kuwajaribu kana kwamba mnapatwa na jambo geni” (1 Petro 4:12). Si ajabu.


Petro alisema kwamba wale wanaoteseka “kwa jina la Kristo” watapata “pumziko” la “Roho wa utukufu na wa Mungu.”

Umewahi kujiuliza utafanyaje katika saa ya majaribio ya mwisho? Yule mwenye bunduki anakutazama na kukuuliza, “Je, wewe ni Mkristo?” Hapa kuna neno kali la kukupa matumaini kwamba unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko unavyofikiri.


Petro anasema, “Mkitukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu na wa Mungu anakaa juu yenu” (1 Petro 4:14). Kitia-moyo hiki kutoka kwa Petro kinasema kwamba katika saa ya tishio lisilo la kawaida (iwe la matusi au kifo) kutakuwa na “Roho wa utukufu na wa Mungu akitulia juu yetu.” Je, hiyo haimaanishi kwamba Mungu hutoa msaada wa pekee katika saa ya shida kwa wale wanaoteseka kwa sababu wao ni Wakristo?


Simaanishi kuwa hayupo kwenye mateso yetu mengine. Namaanisha tu kwamba Petro alijitahidi kusema kwamba wale wanaoteseka “kwa jina la Kristo” watapata “pumziko” maalum juu yao la “Roho wa utukufu na wa Mungu.


Omba kwamba huu utakuwa uzoefu wako wakati majaribu yatakapokuja. Kutakuwa na rasilimali za uvumilivu katika wakati huo ambazoo hatuna wakati mwingine wowote. Jipe moyo.


Wakristo wengi ulimwenguni leo hawajui hatari ya kumwamini Kristo, tumezoea uhuru bila mateso, kana kwamba ndivyo inavyopaswa kuwa.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page