Kwa sadaka moja amewakamilisha hata milele wale wanaotakaswa. (Waebrania 10:14)
Mstari huu umejaa faraja kwa wenye dhambi wasio wakamilifu kama sisi, na umejaa motisha kwa ajili ya utakatifu.
Inamaanisha kwamba unaweza kuwa na uhakika kwamba unasimama ukiwa mkamilifu na kukamilika machoni pa Baba yako wa mbinguni sio kwa sababu wewe ni mkamilifu sasa, bali kwa sababu “unatakaswa,” “unafanywa kuwa mtakatifu”—kwamba kwa imani katika ahadi za Mungu, unajiondoa kutoka kwenye kutokamilika kwako na kuelekea utakatifu zaidi na zaidi. Hii ndiyo maana ya Waebrania 10:14.
Je, imani yako inakufanya uwe na shauku ya kuacha dhambi na kupiga hatua katika utakatifu?
Je, imani yako inakufanya uwe na shauku ya kuacha dhambi na kupiga hatua katika utakatifu? Hiyo ndiyo aina ya imani ambayo katikati ya kutokamilika unaweza kumtazama Kristo na kusema, “Tayari umenikamilisha mbele ya macho yako.”
Imani hii inasema, “Kristo, leo nimefanya dhambi. Lakini naichukia dhambi yangu. Kwa maana umeandika sheria moyoni mwangu, na ninatamani kuifanya. Nawe unafanya ndani yangu lile linalopendaza machoni pako (Waebrania 13:21). Na hivyo, naichukia dhambi ambayo bado ninaifanya; na ninachukia mawazo ya dhambi ninayowaza.”
Hii ndiyo imani ya kweli na uhakika inayookoa. Hii ndiyo imani inayoweza kusema maneno haya kwa furaha, “Kwa sadaka moja amewakamilisha hata milele wale wanaotakaswa.” Imani hii sio majivuno ya wenye nguvu. Ni kilio cha wanyonge wanaohitaji Mwokozi. Ninawaalika, nawasihi, muwe dhaifu kiasi cha kutosha kumwamini Kristo kwa njia hii.
Ninawaalika, nawasihi, muwe dhaifu kiasi cha kutosha kumwamini Kristo kwa njia hii.
Yorumlar