top of page

Uhuru wa Neema

Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa ajili ya pendo kuu alilotupenda nalo, hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo; tumeokolewa kwa neema, akatufufua pamoja naye, akatuketisha sisi pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu. (Waefeso 2:4-6)

 

Hatua kuu ya Mungu katika kuongoka ni kwamba “alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo” hata tulipokuwa “wafu katika makosa yetu.” Kwa maneno mengine, tulikuwa wafu kwa Mungu. Hatukuitikia; hatukuwa na ladha ya kweli ya kiroho au shauku; hatukuwa na macho ya kiroho ya kuona uzuri wa Kristo; tulikuwa wafu kwa yote ambayo ni muhimu kabisa.


Kisha Mungu akatenda - bila masharti - kabla hatujafanya chochote kuwa vyombo vinavyofaa vya uwepo wake. Alitufanya kuwa hai. Yeye kwa enzi alituamsha kutoka katika usingizi wa kifo cha kiroho, ili tuone utukufu wa Kristo (2 Wakorintho 4:4). Hisia au fahamu za kiroho ambazo zilikuwa zimekufa, zilipata uhai kimuujiza.

 

Tendo gani lingekuwa la upande mmoja zaidi, huru kabisa, na lisilohitaji maelewano kuliko mtu mmoja kumfufua mwingine kutoka kwa wafu! Hii ndiyo maana ya neema.

Andiko la Waefeso 2:4 linasema kwamba hilo lilikuwa tendo la “rehema.” Yaani Mungu alituona katika hali ya umauti wetu na akatuhurumia. Mungu aliona mshahara wa kutisha wa dhambi ukitupeleka kwenye kifo cha milele na huzuni. “Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema . . . alitufanya kuwa hai.” Na wingi wa rehema zake ulituzidi katika uhitaji wetu. Lakini cha kustaajabisha sana kuhusu kifungu hiki ni kwamba Paulo anavunja mtiririko wa sentensi yake mwenyewe ili kuingiza, “mmeokolewa kwa neema.” “Mungu . . . alituhuisha pamoja na Kristo — kwa neema mmeokolewa — na kutufufua pamoja naye."

 

Paulo atasema hivi tena katika mstari wa 8. Kwa hivyo kwa nini anavunja mtiririko wa sentensi yake mwenyewe ili kuiongeza hapa? Zaidi ya hayo, mkazo ni juu ya rehema ya Mungu inayojibu masaibu yetu ya kufa; basi kwa nini Paulo anatoka katika njia yake kusema kwamba pia ni kwa neema kwamba sisi tumeokolewa?

 

Nadhani jibu ni kwamba Paulo anatambua kwamba hapa kuna fursa kamili ya kusisitiza uhuru wa neema. Anapoeleza hali yetu ya kufa kabla ya kuongoka, anatambua kwamba watu waliokufa hawawezi kutimiza masharti. Ikiwa wataishi, lazima kuwe na tendo lisilo na masharti na la bure kabisa la Mungu kuwaokoa. Uhuru huu ndio moyo wa neema.

 

Tendo gani lingekuwa la upande mmoja zaidi, huru kabisa, na lisilohitaji maelewano kuliko mtu mmoja kumfufua mwingine kutoka kwa wafu! Hii ndiyo maana ya neema.


Comments


bottom of page