Wakati Wewe Huwezi Kufa
- Dalvin Mwamakula
- Jan 27
- 1 min read

Kulipopambazuka, Wayahudi walifanya hila na kujifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala kunywa mpaka watakapomuua Paulo. (Matendo 23:12)
Vipi kuhusu wale wenzetu wenye njaa ambao waliahidi kutokula mpaka wawe wamemvizia Paulo?
Tunasoma kuwahusu katika Matendo 23:12, “Kulipopambazuka, Wayahudi walifanya njama na kujifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala kunywa mpaka watakapomuua Paulo.” Haikufanya kazi. Kwanini? Kwa sababu mfululizo wa matukio yasiyowezekana yalitokea.
Mvulana aliisikia njama hiyo.
Mvulana huyo alikuwa mtoto wa dada yake Paulo.
Mvulana huyo alikuwa na ujasiri wa kwenda kwa akida wa Kirumi aliyekuwa akimlinda Paulo.
Jemadari alimsikiliza kwa umakini na kumpeleka kwa mkuu wa baraza.
Mkuu wa baraza alimwamini na akatayarisha “askari mia mbili, pamoja na wapanda-farasi sabini na wapiga-mikuki mia mbili” ili wampeleke Paulo mahali salama.
Paulo hakuweza kufa kwani alipaswa kutoa ushuhuda wake wa mwisho, na Kristo alihakikisha hivyo. Wewe pia una ushuhuda wa mwisho wa kutoa, na hautakufa mpaka uutoe.
Kila moja ya matukio hayo yalikuwa magumu sana kuwezekana. Ni ajabu. Lakini ndicho kilichotokea.
Wale watu wenye njaa waliokuwa wamevizia walikuwa wamepuuza nini? Walishindwa kutathimini kile kilichotokea kwa Paulo kabla tu ya kufanya njama yao. Bwana alimtokea Paulo gerezani na kusema, "Jipe moyo, kwa maana kama ulivyoshuhudia mambo ya hakika juu yangu huko Yerusalemu, vivyo hivyo imekupasa kutoa ushahidi huko Roma pia " (Matendo 23:11).
Kristo alisema Paulo alikuwa anaenda Roma. Na hiyo ilikuwa hivyo. Hakuna shambulio lolote linaloweza kusimama dhidi ya ahadi ya Kristo. Mpaka alipofika Roma, Paulo alikuwa hawezi kufa. Kulikuwa na ushuhuda wa mwisho uliotakiwa kutolewa. Na Kristo angehakikisha kwamba Paulo angeutoa.
Wewe pia una ushuhuda wa mwisho wa kutoa. Na wewe hautakufa mpaka uutoe.
Comments