JINSI KANISA LINAVYOONESHA UZURI WA KRISTO
Injili ni ujumbe wa kitheolojia. Lakini ujumbe huu pia huunda uzuri wa kibinadamu
—uhusiano wa kupendeza ndani ya makanisa yetu, ukidhihirisha utukufu wa Kristo
ulimwenguni leo.
Katika kitabu hiki cha wakati muafaka, Mchungaji Ray Ortlund anathibitisha
kwamba mafundisho ya injili huunda utamaduni wa injili. Katika makanisa mengi,
uzuri wa utamaduni wa injili ndilo jambo linalokosekana kama kipande cha fumbo.
Lakini pale injili inapopata nafasi ya kuonyesha nguvu zake kikamilifu, kanisa
hugeuka kuwa lenye mng’ao wa utukufu wa Kristo.
“Kitabu kinachovutia. Kinachoshawishi. Kinachotia moyo. Kinachochunguza kwa
undani. Na zaidi ya yote, kinachoteka hisia. Ni maono mazuri ya jinsi kanisa
linavyoweza kuwa kupitia nguvu za injili.”
THOMAS R. SCHREINER, Profesa wa Tafsiri ya Agano Jipya, James Buchanan Harrison,Chuo Kikuu cha Theolojia cha Southern Baptist
“Ortlund anaunganisha tafakari za kina za kibiblia kuhusu jinsi mafundisho ya injili
yanavyopaswa kuzaa utamaduni wa injili, akitumia nukuu zilizochaguliwa kwa
uangalifu kutoka kwa watakatifu wakuu wa historia ya kanisa. Hiki ni kitabu cha lazima
kusomwa na kila kanisa linalotaka kusaidia, badala ya kuzuia, waliopotea kuvutiwa na
Kristo.”
CRAIG L. BLOMBERG,Profesa Mashuhuri wa Agano Jipya, Seminari ya Denver
“Katika kitabu hiki chenye makali, Ortlund anafanya kazi muhimu na ya kuvutia ya kuunganisha injili inayotoa uzima na uzoefu wa maisha na ushuhuda wa kanisa.”
STEPHEN T. UM, Mchungaji Mkuu, Kanisa la Presbyterian la Citylife, Boston, Massachusetts
RAY ORTLUND (PhD, Chuo Kikuu cha Aberdeen) ni mchungaji wa Kanisa la
Immanuel huko Nashville, Tennessee. Yeye ni mwandishi wa vitabu kadhaa,
vikiwemo Preaching the Word chenye maelezo ya vitabu vya Mithali na Isaya, na pia
ni mchangiaji wa ESV Study Bible. Pia, ni rais wa Renewal Ministries na anahudumu
kwenye mabaraza ya The Gospel Coalition na Acts 29 Network.
Injili: Jinsi Kanisa Linavyoonesha Uzuri wa Kristo
Ray Ortlund
We do not provide refunds or accept returns for purchased books. However, we are committed to addressing any issues related to manufacturing defects in the books you receive.